Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi Peter Robert Kilave wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari ya Kata Tushikamane ya mjini Morogoro baada kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la Insha kuhusu Ujenzi wa Miundombinu Afrika Mashariki.Mwanafunzi Peter amechukua ushindi wa kwanza kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wan chi tano za jumuiya ya Afrika Mashariki .
Peter alipokea tuzo hiyo wakati wa Mkutano wa wa kuu wan chi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Speke’s Bay Resort,Munyonyo, Kampala Uganda juzi.Kutokana na ushindi huo Mwanafunzi huyo amepewa tuzo ya dola za Marekani 1500, na cheti na alikabidhiwa zawadi hizo na mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera Peter Robert kwa ushindi huu.

    ReplyDelete
  2. Congratulation" kwa kazi nzuri na ya kupendeza pia kwa Wantzania!

    ReplyDelete
  3. Emanuel P. M.December 03, 2013

    Isingekuwa uwepo wa shule hizi za kata zinazolalamikiwa sana kwa mapungufu yake mpaka wengine wanashauri zisingeanzishwa huyu Peter Robert Kilave angeishia wapi ? hongera serikali yetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...