National Geographic ya Washington, DC siku ya Jumatano, Dec 11, 2913 walionyesha vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye mbuga zetu za wanyama kwa wahudhuriaji ambao wengi wao walikua Wamarekani pia ulialikwa Ubalozi wa Tanzania akiwemo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba,
Mhe. January Makamba akitoa shukurani zake kwa Nafional Geographic kwa jitihada zao za kusaidia kutangaza hifadhi za Taifa za wanyama pori/
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwapongeza National Geographic kwa kuwa Mabalozi wa Tanzania nchini Marekani na kuahidi kufanya nao kazi kwa karibu zaidi na mlango wa Ubalozi wa Tanzania upo wazi pindi wanapohitaji msaada.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi nae akiwapongeza National Geographic kwa jitihada zao za kutangaza mbuga za wanyama pia aliwahakikishia wahudhuriaji Tanzania ndio mahali pekee kwenye vivutio na aina nyingi ya wanyama hao.
Andrew Evans mfanyakazi wa National Geographic ambaye ndiye aliyetembelea mbuh=ga za wanyama Tanzania, akiwaonyesha wahudhuriaji picha mbalimbali za wanyama na kuwaelezea kuhusu Tanzania kwamba ni nchi ya Amani na Utulivu na Watanzania waliojaa na upendo kwa kila mtu.

Akianza kuelezea alianza kuwaonyesha Khanga kwamba hutumika kwenye shughuli nyingi na kwamba utaiona kila pahala,
Pia alionyesha picha ya kukutana na marafiki zake hao kwenye picha na yeye alipewa jina la Mzungu, Andrew Evans anaufahamu mkubwa wa hifadhi za Taifa jinsi alivyozielezea na vitu vilivyomo lazima uatatamani kuelekea huko kesho.
Mhe. January Makamba akimpongeza Andrew Evans kwa jinsi anavyoitangaza Tanzania.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mhe. January Makamba wakiongea na wahudhuriaji walijaribu kudadisi mambo mengine kutoka Tanzania na kuahidi kuja nchini Tanzania kutembelea mbuga za wanyama.
Mhe. January Makmba akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula ndani ya thieta za National Geographic, Washington, DC.
Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Afisa wa Ubalozi Mindi Kasiga, Mkurugenzi mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wahudhuriaji wengine waliofika National Geographic ya Washington, DC. Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. National Geographic Society ikikutangaza ujue unavyo Viwango.

    Halafu ndugu zetu Kenya, Uganda na Rwanda wanataka tutumie Visa moja kwa Utalii na sisi wakati Viwango vyao Sekta ya Utalii vipo chini!

    Ktk Afrika ya Mashariki tutaungana kwa baadhi ya mambo lakini mengine hapana.

    ReplyDelete
  2. Jamani mbona theater tupu? Wabongo Washington wako wapi!

    ReplyDelete
  3. Lakini jipya lipi hapa National geographic chanel inaonesha miaka yote wanyama ngorongoro.Mwaka 2004 naingia europe National geographic ni miongoni mwa my favorite chanel na vitu vyote vinaoneshwa tena wakati mwengine unapata matangazo kupitia tafsiri kwa lugha mbalimbali .

    ReplyDelete
  4. tatizo letu ni kwamba kuna idadi kubwa ya watalii wanaokuja tanzania ambao huteremkia uwanja wa ndege wa nairobi. tupambane kuhakikisha kuwa kila mtalii anayetaka kuja tanzania anatua na ndege kia au dia.

    ReplyDelete
  5. Mtz anapaswa kuwa 'mjasiliamali'au
    mtundu inapofikia kutangaza/kuuza mawazo ya mbuga zetu.Ila wakati mwingi ni serikali iliyolala inayotuangusha.Kwa nini watalii wasiwekewe vivutio wajapo nchini moja kwa moja; kwa mfano kutoa punguzo la tozo au bei za hoteli na viingilio.Tusikimbilie kulaumu wenzetu wa Kenya wakati nao wana ubia nasi; yaani nyumbu n.k. ambao huhama na msimu bila kujali mipaka.Ugonvi huu hauna tija.

    ReplyDelete
  6. Wanamuziki wa Kizazi Kipya mpo wapi?

    Mlitakiwa muwe mnatangaza Utajiri huu wa Utalii wetu badala la kuandaa mashairi mengi ya Mapenzi, na mipango ya mapesa mengi na matatizo ya maisha.

    Igeni mfano wa ndugu zetu wa miaka ile ya 1984 Varda Arts walioimba Kibao chenye vionjo hivi hapa chini kuwakaribisha Wageni nchini Tanzania:

    Wimbo:
    WAGENI KARIBUNI TANZANIA, NCHI YENYE AMANI NA UZURI

    JAMBO, HABARI GANI NZURI SALAMA TANZANIA, TANZANIA X 3.

    ReplyDelete
  7. Tunafurahi sana kwa Jitihada kubwa za baadhi ya viongozi wetu hadi tunapata yote haya!

    Isipokuwa Tanzania tuna Utamaduni mbaya sana wa kuto wajibishana endapo anatokea mmoja wapo anahujumu licha ya maendeleo kama haya kuwagharibu jitihada kubwa sana Viongozi wengine.

    Sio siri kila penye Maendeleo ama mafanikio kwamwe hapakosi wapinga maendeleo!!!

    ReplyDelete
  8. Mdau wa 2 juu,

    Theatre ipo tupu Wabongo wapo buzy kwenye ubebaji wa Maboksi !!!

    ReplyDelete
  9. Mtoa Maoni wa Pili juu,

    Wabongo wanashiriki Hafla za Ubalozi wa Tanzania Washington-DC endapo wataahidiwa uwepo wa Misosi ya Tanzania kama Ugali kwa nyama choma na Chai za michaichai kwa Vitumbua Maandazi na Chapati!

    Inaokenana Mhe. Mama Mulamula hakufafanua maandalizi kwenye Shughuli na ndio maana Ukumbi upo wazi!

    ReplyDelete
  10. Ahhh Watanzania Marekani hii ni aibu!

    Yaani nchi inatangazwa Kiutalii ninyi mpo buzy kwenye kubeba maboksi?

    ReplyDelete
  11. Hahahaha !

    Acha nicheke Mdau wa 5, ni kuwa sisi Tanzania na Kenya tukibishana kwa Siasa na Uchumi huku tukifikia kutengana wenzetu wanyama Nyumbu na Nyati wala hawana habari ndio kwanza Msimu ukibadilika wanafunga virago wanahamia nchi nyingine!

    Isipokuwa Watafiti wa Wanyamapori kutoka Ujerumani wamefuatilia wametoa Ripoti ya kuwa wanyama wanakwenda Kenya kwa muda mfupi tu kwa mwaka (kwa miezi kama mitatu 3 hivi wanakuwa uhamishoni) wakati Makazi yao ya kudumu ni Tanzania wanakokaa kwa muda mrefu zaidi katika kipindi cha mwaka kama miezi 9 hivi na pia ndiko wanakozaliana !

    Hivyo KAMA INGEKUWA NI SUALA LA KUWAPA URAIA WANGEKUWA WATANZANIA!,,,(HII HATA WAO KENYA WANAJUA).

    KAMA NI UBIA MAIN SHARE HOLDER (MBIA MKUU ATAKUWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA ZAIDI YA 51%+ SHARES)

    NAWAKILISHA:

    (MSIJE MKASEMA AMENITUMA RAISI KIKWETE KUJITETEA UMILIKI WA WANYAMA KWA TANZANIA)

    ReplyDelete
  12. Mdau hapo juu nakuunga mkono, Wabongo hawakufahamishwa malaji hayao na hasa uwepo wa "senene" wa bure. Mdau mwingine kataja "dia" siku hizi ni JNIA=Julias Nyerere Internatinal Airport. Jitahidini kuwa mnarudi kwenu, mnapitwa na mengi ooohooooo shauri yenu.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...