Ajali mbaya iliyohusisha magari mawili makubwa (malori) imetokea leo katika eneo na mteremko wa mto Wami,Mkoani Pwani na kupelekea msongamano mkubwa wa magari mengine yakiwemo mabasi yaendayo mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha pamoja na yale ya nchi jirani.
Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni kufeli kwa breki kwa moja ya malori hayo yakiwa yanateremka kwenye mlima huo.Askari Polisi wapo eneo la tukio kuhakikisha usalama unapatikana na kutafuta namna ya kuyapitisha magari mengine.haijafahamika ni watu wangapi wamepoteza maisha ama kujeruhiwa.
Pichani ni Malori hayo yaliyogongana yakiwa yameziba njia baada ya kugongana eneo la mto wami.Picha na Mdau wa Globu ya Jamii alie safarini.
Michuzi Hongereni sana - you are doing the a nice job.
ReplyDeletekwanni madereva mnashindwa kibadili tabia na kufuata sheria hivi ni nani aliye waloga
ReplyDelete