Kwako michuzi na wato wote wanaoitakia mema nchi yetu, 
Naandika hii nikiwa na hasira iliyochanganyika na majonzi. Yaani hata sijui nianzie wapi. Awali ya yote naomba urudishe ukurasa wa kwanza zile picha za uharibifu wa barabara ulizoposti majuzi. 
Mimi niko hapa Sao Paulo huku Brazil. Nilistushwa sana sana na picha hizo pamoja na maelezo yake, kadhalika na maoni ya wadau wako. Ni dhahiri wengi ya wadau wako aidha ni kuendeleza tu tabia ya kubeza na kuponda kila kilicho mbele yao ama ni kwa sababu hawana habari ya kinachoendelea. 
Katika research niliyofanya katika mitandao ya kijamii na ya magazeti juu ya swala hilo, nimejikuta nafikia mahali kuamini kuwa swala hili halina tofauti na lile la Operesheni Tokomeza, ambapo mawaziri wane wamemwaga unga hivi hivi kiutani utani, japo hawahusiki moja kwa moja. Hii inaitwa uwajibikaji. 
Siku chache baadaye nimesoma Wizara ya Maliasili na utalii ikitamka kuwa baada ya kusitishwa kwa Operesheni Tokomeza, Tembo wawili huuwawa na majandili kila siku. Hii haiukubaliki, kilichokosewa na kirekebishwe haraka na ianze tena kama alivyoahidi JK. 
Kwa upande wa barabara sioni kama kuna sababu ya Waziri Magufuli awajibike, kwa maana yeye amekuwa mstari wa mbele kusimamia sheria kibao kamataarifa hii niliyosoma mahali kuwa Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, amesema ataendelea kusimamia sheria ya barabara namba 30 ya mwaka 1973 hadi anaingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara.
 “Nchini Ujerumani, uzito wa magari yote ni tani 40, Uingereza tani 40, Ufaransa 40, Urusi 38 lakini Tanzania tani 56, wakati mwingine tunakamata hadi tani 96,” aliongezea kwa kuwaga data kama kawaida yake katika taarifa hiyo. 
Hata hivyo nimesoma mahali pengine tena kuwa miezi miwili iliyopita Waziri Mkuu alisema sheria hiyo ilegezwe ili tume iundwe. Yaani magari yenye uzito yaendelee kutanua tukisubiri tume! 
JAMANI! HIVI KWELI TUSUBIRI TUME IUNDWE WAKATI BARABARA ZINAKUFA HIVI HIVI TUNAANGALIA KWA MANUFAA YA WACHACHE??? LET’S BE SERIOUS FOR ONCE! 
Hilo kaka halikubaliki. Nashauri wakati tume hiyo ikisubiriwa kuundwa (hata sijui ya kazi gani katika kuzuia uharibifu wa barabara, maana data hapo juu zinatusha) Dokta Magufuli aruhusiwe aendeleze juhudi zake za kukomboa barabara zetu. 
 Nasema hivi kwa sababu kama ilivyo katika kusitishwa Operesheni Tokomeza, barabara zetu zinaangamia kwa kilomita kibao kila dakika. Nimesoma mahali pengine kuwa gharama za kukarabati hizo barabara zilizoathirika kwa uzito wa magari ni takriban dola bilioni 350 ambazo ni hela za walipa kodi. Hili halikubaliki asilani!!! 
Namalizia kwa kumuomba Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda afikirie upya swala la kulegeza sheria. Hapana. Asifikirie bali achukue hatua za haraka sana chini ya kauli mbiu ya BIG RESULTS NOW! 
Mdau Nehemia
Sao Paulo, Brazil
 Taswira hizi ni za barabara ya Morogoro road ambako sehemu kibao zimeharibika bila shaka kutokana na  uzito wa magari. Mwenye data atusaidie....





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. siku nyingine mwandishi aandike barabara ya morogoro sio barabara ya morogoro road...

    ReplyDelete
  2. sehemu gani hapo? kama ni Mlandizi mpaka Chalinze ni kwamba barabara ni ya muda mrefu huwa inakarabatiwa tu haijajengwa upya kama inavyotakiwa. vipande vya dar - mlandizi na Chalinze kuendelea segera au Moro vimejengwa si muda mrefu

    ReplyDelete
  3. Wataalam wa ujenzi wa barabara tusaidieni ni ujenzi hafifu au uzito kuzidi ili tuchangie vizuri hii issue ambayo ilileta kizaazaa kati ya WM na Waziri Magufuli ingawa Rais JK alikuja kuitolea ufafanuzi(wa akili sana) wakati akifungua ujenzi wa moja ya barabara huko mkoani Geita miezi michache iliyopita.

    Binafsi kwa kutumia Physics yangu ndogo naona ni Uzito umezidi.Lami inabonyea kwa DUCTILE syle siyo BRITTLE style au siyo Engineers?Hee hee kweli kila mtu na fani yake.

    David V

    ReplyDelete
  4. Tumebadili mawaziri sana wa ujenzi,tulikuwa na magufuri,tukapewa chenge,tukapewa mramba ,mara shukuru,tena tukapewa magufuri.Tujiulize sehemu hii ilijengwa chini ya waziri gani?wenye data tujuzeni

    ReplyDelete
  5. uzito mkubwa wa magari ndio unaochangia uharibifu wa barabara,...suluhisho ni kuimarisha reli tu..

    ReplyDelete
  6. Uharibifu huu unatokana na mzigo mkubwa na magari mengi. Ona upande wa pili wa barabara kurudi Dar upo safi kwa vile mzigo ni kidogo. Reli ikiimarishwa itapunguza magari barabarani na uharibifu utapungua.

    ReplyDelete
  7. jamani tumechoka na uowongo na utapeli wa makandarasi je serikali iko wapi? kwanini msifanye kazi nzuri au mlinunua vyeti? pesa unazojilimbikizia haziwezi kukuzika watu ndo watakuzika, thamini maisha ya watu. au mpaka tutoe wataalamu toka nje? tuliwapa mikopo ya kusoma nayo hamjarudisha nyie mnaangalia kuiba tu. ebu mue wawazina utendaji wa kazi. ahsante

    ReplyDelete
  8. Duuh unauliza majibu!kila kitu kipo wazi kabisa kwanza ni ujenzi mbovu,pili magari yenye uzito mkubwa ndio yanamalizia kuharibu kabisa. Hiyo ndo Bongo

    ReplyDelete
  9. Kama ni uzito, uzembe sio watu wa mzani wala madereva. Ni wizara, si ilijuwa kuwa barabara hii inapirika nyingi kuliko zote za nchi hii, na si walijuwa makisio na uzito wa magari yanayopita, na si walijuwa kuwa wemgine huzidisha uzito, sasa lazima wangekuwa na vigezo na taarifa hizo kabla ya kumpatia conractor hiyo tender. Mhh!. Lakini bado, wenye uwelewa tupeni jibu la kisanyansi.

    ReplyDelete
  10. Asalam alyekum wapenzi wa blog ya michuzi. Napenda kutoa maoni yangu japo cna ujuzi, lakini hapo hata kipofu ataona. Hiyo inatokana ujenzi kiwango chini sana kwani wakati wakijenga si wanajua kama hiyo ni barabara kuu inapita gari aina zote. Hii kwei nchi imefanywa kama kichwa cha mwenda wazimu Lakinni ikumbukew kuwa wapatao tabu ni wananchi

    ReplyDelete
  11. Nionavyo hali hii ya barabara imesababishwa na uzito hasa uliozidi,pia na ujenzi wa kiwango cha chini

    ReplyDelete
  12. Mimi ni Mhandisi (Engineer) naomba niwaeleweshe nini kinaendelea ktk barabara zetu tunazozijenga kwa gharama kubwa:

    1. Barabara ina design yake ya kuhimili mzigo (pavement design)hivyo basi uzito wa magari hutakiwa kuzingatia uwezo wa barabar yenyewe ndo maana kukawa na mizani

    2. Ujenzi wa barabara zetu hufuata maanadalizi, maadili na taratibu zote za kihandisi, ndiyo maan utaona barabara ikishakamilika kujengwa huwekwa katika kipindi cha uangalizi/matizamio kisichopongua miaka miwili, ikitokea barabara ikaharibika basi mhandisi mshauri na mkandarasi watawajibika kurudia ujenzi wa barabara husika kwa gharama zao, mfano ni ile barabara ya Kilwa. Hivyo ni vigumu sana kujenga baraba chini ya kiwango.

    3.Nchi zilizoendelea hujenga barabara zake na tena zenye ubora kuliko zetu (Asphalt Concrete) ni tabaka la lami zuri kabisa. Katika barabara zao uzito ni mdogo ukilinganisha na sisi, mfano Marekani ni tani 36.2, Uingereza tani 40, Ujerumani tani 40, Ufarasa tani 40, Urusi tani 38, lakini kwa Tanzania ni tani 56 ambacho ni kiwango kikubwa sana.

    4. Kuna utafiti umefanyika hapa Tanzania na umeweka wazi kuwa barabara zetu zinaharibiwa na wafanya biashara wasioitakia mema nchi kwa kuwa wanatumia tairi zijulikanazo " Super Single Tires" ambazo ni adui mkubwa sana kwa uharibifu wa barabara, simple physics, Pressure between two surfaces "the smaller the area the greater the pressure" malori mengi sana wa hao wafanyabiashara yana hizo tairi na bado yanazidisha uzito wewe unategemea nini kwa barabara iliyojengwa kuhimili Dual Tires (Tairi mbili kwa pamoja). Hapo barabar zitatoboka na ndicho hicho mnachokishuhudia ktk picha, na bado yatatokea madhara makubwa kuliko unavyoona kama serikali itaendelea kuwakikingia kifua wafanyabiashara waroho kuzidisha uzito.

    5. Hitimisho, Serikali itafakari upya kuzuia kuwadhibiti wasafirishaji (Transporters) kwa kutumia sheria namba 30 ya mwaka 1973 ya usalama barabarani. La sivyo barabara tunazozijenga si lolote zitakwisha harahaka sana na wala tusisingizie eti zimejengwa kwa viwango duni- never!!!

    ReplyDelete
  13. tuna watanzania maarufu wa ujenzi wa barabara international wakipewa hiyo bahati ya kufanya hiyo kazi ni tutaona maajabu tatizo ni watu wa kawaida inabidi watafutwe. huu ujenzi ni utani na kutokuwajibika hii ni aibu kwa uongozi uliopo. uzembe uvivu rushwa na kutowajibika hakua exucuse hapa.

    ReplyDelete
  14. Majibu ya Mhandishi, Sirikali ikizingatia ndo suluhisho.

    ReplyDelete
  15. ASANTE ENGINEER, HIZO TAIRI SUPER SINGLE HAPA UK NDO TAIRI WANAZOTUMIA KWENYE MA TRAILER YA MIZIGO. TATIZO HAPO SIO TAIRI NI HIZO TOFAUTI ZA TANI, NINA DEREVA NINAYEMJUA HAPO BONGO ALISHASAFIRI NA MZIGO WA TANI 80 KWA KUTOA RUSHWA KILA MIZANI. MATOKE NDO HAYO!!

    ReplyDelete
  16. Alijisemea Issa Michizi"tazama mkeka huo" teehteeh....bongo tambararezz.

    ReplyDelete
  17. Kwa nchi zetu za kiafrika na umaskini ndicho chanzo ya haya yote,utajiri wa haraka haraka, pesa bila jasho. Bila kupoteza muda nadhani umefika wakati wa kuachana na mizani badala yake vijengwe vibande vya barabara kwenye kila mizani au ka vile geti ili magari yanayozidi uzito unaotakiwa yasiweze kuendelea na safari kwa sababu ya kutitia. Hii ni suruhisho la kuduma. Hakuna Mizani hakuna rushwa, hakuna afande wenyewe watajuta.Hii sijaona wala kusikia sehemu nyingine lakini kwa Tanzania tukiwashirikisha wataalamu wetu ni njia nzuri.
    Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  18. Thanks Mr. Engineer....nimejifunza kitu kikubwa sana...!

    ReplyDelete
  19. Nakujibu anonymous uliyetaja super single za UK:

    Kuna namna mbili za kutumia hizo super single hapa kwetu hawa transporters hutemper na air booster ambazo kimsingi huharibu zaidi barabara na huepuka kutumia Mechanical suspension system kwenye rear axles kwa vile ni ngumu kutemper nazo. Ningekupa shule ya kutosha ili ujue nini namaanisha lakini bahati mbaya hapa sina muda huo kwa sasa.

    ReplyDelete
  20. Mkapa na Kikwete mmjitahidi kutuwekea barabara Tanzania ilikuwa sasa inaongoza kwa barabara kwa nchi za africa mashariki na kati. Lakini kwa mtaji wa tani 80 kupita kwenye barabara hayo ni majanga. Suluhisho ijengwe reli ndio barabara zetu zitadumu vinginvyo hakuna kitu miaka 10 ijayo!!

    mdau arusha.

    ReplyDelete
  21. Mdau wa Sao Paulo, Brazil umenena jambo kubwa sana, kwa kuwa Ujenzi wa Miundombinu hii haupatikani bure ni mojawapo ya hayo matatu chini:

    1.Mikopo ambayo hulipwa kwa Riba huku riba hiyo hutokea kwenye Kodi tunayotozwa sisi wananchi.

    2.Misaada ambayo haipatikani bure, Kanuni ni kuwa ukitoa NDOBE unapata KIBABA CHA UNGA!

    3.Fedha za Kodi tunayotozwa sisi wananchi kama ilivyokuwa Riba ya Mikopo tunavyoilipa.

    HAKUNA BURE, NA MARA ZOTE BURE GHALI!!!

    ReplyDelete
  22. kwa upande wa morogoro road hukuna aina hiii sema kashindwa kutofautisha hapa ni mkoa wa morogoro ukimaliza mbuga ya mikumi unaanza milima ya iovyi na ukimaliza magubike njia ya dodoma

    ReplyDelete
  23. Ingependeza pia hoja hizi ziwe na mtu wa kufanya summary na kupeleka kwa watu wa magazeti ili isambae kwa wasio na mtandao, kero hii ingewakuna vichwa wengi - tuna kitu cha muhimu kujadili hapa kuokoa nchi yetu kiuchumi na kwa usalama wa barabarani maana hayo matuta ni balaa kwa ajali!

    ReplyDelete
  24. The mdudu,anasema mm kilio changu ni kwa wafanya biashara wakubwa hao ndio mapapa ya kuogopwa maana hawashikiki wengi wao ni wadosi na waarabu,wao idara zote PESA TALK yaani inaniuuma sn kumbe mtikila alikua anaona mbali sn huyo mzee wa watu,,mpaka mie mwenyewe enzi hizo nilikua nasema eti mbaguzi kumbe ule ulikua utoto wangu tu,kumbe ukweli ni wao ndio wabaguzi namba moja duniani,mjomba Michuzi plz usiibanie hii wacha nitoe yalio mayoni coz inaniuma sn kuona wao wanatesa kwa rushwa zao huku wimbi la watanzania wakiteseka,,na hili tuliangalieni kwenye katiba yetu ya TANGANYIKA asanteni sn wajumbe wa tume ya katiba,

    ReplyDelete
  25. HODIHODI WADAU WA BLOG YETU TUKUFU ISSA MICHUZI!!!

    NILISHAA WAHI KULISEMA HILI MWAKA 2011 KWA NINI MTU ANAHARIBU BARABARA KWA KUZIDISHA UZITO? KAMA NI MIMI NISINGERUHUSU GARI LIONDOKE NA MZIGO ETI KWAKUWA KALIPA FAINI BADALA YAKE ASILIPE FAINI BALI APUNGUZE HUO MZIGO KISHA AENDE ASHUSHE AIJIE ULIOBAKI. HIYO FAINI AMBAYO ANGELIPA TUWALIPE WALINZI WA MZIGO KWA RIBA. NAMAANISHA KUWEKO NA KIWANGO CHA MDA WA KUIJIA MZIGO ULIOACHWA NA MDA UKIZIDI UNALIPIA WAITING CHARGE. NI ADHABU TOSHA SIDHANI KM KUNA MFANYA BIASHARA ATAKAE PENDA KUPATA HUO USUMBUIFU, LAKINI SWALI LINAKUJA JEEE YUUU WAPI AFISA MWAMINIFU WA KUWEZA KUMUWAJIBISHA DEREVA ASHUSHE AU YUUU WAPI MLINZI MUAMINIFU ASIE WAZA KUJIMEGEA KWENYE MZIGO ALIOACHIWA BASI UTAONA KUWA BONGO NI MAJANGA MATUPU MAANA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA IMESHIKA KASI..

    WAKO MDAU KUTOKA KUMASI NGARA.

    ReplyDelete
  26. Kuwasha moto/ mioto ovyo pamoja na ajali za magari kuungua mto pia ni sababu ya barabara hii Kutepeta/kunyeyuka lami ya barabara hii ya Morogoro Road.

    Jibu ni kuimaisha usafirishaji wa mizigo mizito, mafuta n.k kwa njia ya reli ya kati-TRL/Tazara ili barabara zisiungue moto kwa maroli ya mafuta kuungua moto na pia magari mazito yapigwe marufuku kutumia barabara.

    Mdau
    Mikumi, Morogoro.

    ReplyDelete
  27. Naomba nichangie tena.Kwani hao wasafirishaji hawaelewi kwamba barabara inapoharibika na wao wataumia maana barabara ikiwa mbovu magari yao na uzito huo yatavunja hizo springs/boosters na kuharibu vifaa vingine.Gharama ya Matengenezo itaongezeka.Muda wa safari utakuwa mrefu,safari ya siku 2 itatumia siku nne,gharama za mafuta zitaongezeka,posho za madereva/conductors zitaongezeka.nk

    Serikali ikae na hawa wasafarishaji iwape 'shule' ya kutosha kuhusu umuhimu wa barabara hizi.Wao wataondoka,Tanzania itabaki.Na wengi wa hawa wasafirishaji ni SHULELESS lakini wana pesa ya kutisha.Mwisho

    David V

    ReplyDelete
  28. Hebu jamani tuangalie hivi hiyo pesa wanayotozwa faini inatosha kulipia gharama za ukarabati utakaofanyika hapo? Na tulipo waruhusu waendelee kuharibu mpaka hapo tutakapo jipanga vizuri, je tunazo pesa za kukarabati wakati huo au ndiyo kujiongezea mikopo kwa uzembe wa wengine kutowajibika? Kama tutaishia kutumia pesa zetu kukarabati barabara na kuendelea kulipia matatizo yanayotokana na uzembe wa makusudi watu wengine itakuwa ndoto kwetu kufikia maendeleo ya kweli. Hebu tuwe makini tusibebeane uzembe kwa kiwango hiki na wala hakuna haja ya kumwogopa mfanyabiashara wa usafirishaji. Waelimishwe kwanza kwa kutumia mbinu zote mpaka za flash sms na baadaye tuwabane. Faida wapate wengine, tutengeneze barabara na jasho la wengine ni haki kweli?

    ReplyDelete
  29. Mimi naona bora barabara zote ziharibike malori yashundwe kupita labda ndo reli itatengenezwa

    ReplyDelete
  30. Inauma kweli kuona hali ya miundombinu yetu inavyoharibika. Kitaaluma ni mhandisi na najua ni namna gani lami inavyofanya kazi. kwa kiswahili rahisi ni mfano wa bigG au springi. Gari moja laweza tosha kabisa kuharubu barabara ambayo ilikadiriwa itumike miaka 20 bila matengenezo. Iwapo springi ukiivuta hadi kupitiliza kiasi ambacho kinatakiwa ili irudie hali yake haijalishi umevuta mara ngapi. Mara kadhaa nimeshuhudia baadhi ya mabasi ya mkoa yakifaulisha abiri karibu na mizani na watu wapo radhi kabisa. Hi niaibu kwakuwa wakati mwingine na sie wananchi tunachangia.Inasikitika kuona reli ya kaskazini imesahaulika kabisa. Kwa nchi kama Tz reli ndio suluhisho, baada ya uhuru imejengwa reli moja na zile wazotuachia wakoloni nazo turasubiri filimbi ipulizwe watu tuanze kung'o mataruma kwaajili ya biashara ya vyuma chakavu.

    ReplyDelete
  31. La muhimu hapa pia ni sisi wote Wananchi, Wasafirishaji na Maafisa wa Mamlaka zetu kuelewa ya kuwa

    1.Miundombuni inatugharimu sana.
    2.Miundombinu inajengwa ili kutuwezesha sisi kufikia maendeleo.

    Hivyo tuzingatie ya kuwa tunailipia na pia tuitunze ili ituhudumie zaidi wa gharama za chini!!!

    ReplyDelete
  32. Tatizo hwa wau wanaosaini mikataba ya ujezi, hawafuatilizii ujenzi wenyewe au kuteua watu wataalam engineers wa nje ya kampuni kuhakikish kuwa nyakati zinazotumika katik ujenzi ni sawa na ni za kitaalam. mara nyingi huku ulaya kutengeneza barabara zote za lmi, huwa wanatumiaga mawe makubwa kwanza kujaza barabara, then kokoto juu yake then kushindilia na magreda, kwa kutumia ujenzi kwa staili hii inasaidia barabara utodidimia kama hivi, pia uchanganyaji wa lami na kokoto katika hiyo lami, huwa kokoto inakuwa nyingi zaidi kulikoni lami yenyewe, maana lami ikizdi ni rahisi kuyeyuka wakatu wa jua kali, na kupinda pinda.

    Mdau Engineer ktk ujenzi nchini Finland.

    ReplyDelete
  33. MIE MWENYEWE NAUMIA KAMA MTANZANIA KUONA BARA BARA ZINAHARIBIWA KWA MAKUSUDI WAKATI MAMLAKA HUSIKA ZIPO!!
    KWA NINAVYOFAHAMU MIE KWANINI MIZIGO MIZITO USISAFRISHWE KWA TRENI KAMA YA KWENDA ZAMBIA TAYARI KUNA RELI YA TAZARA,NA MIZIGO YA KWENDA KONGO KUNA RELI YA KATI SASA KWANINI YAANI WANAANGALIA TU IBAKI TU KUSAFRISHA MIZIGO MICHACHE KWENYE SEHEMU AMBAZO HAKUNA RELI,NASHINDWA KUELEWA HAPA HIVI KUNA WATU WANAOFANYA KWELI TZ KWELI KWA HALI HII BARA BARA KAMA WAHUSIKA WAMEKUFA VILE,IMALISHENI RELI KUPITISHIA MIZIGO BANDARI YA KIGOMA IIMARISHWE TENA KUNUSURU BARA BARA HIZI.RAIS ANAJENGA BARA BARA ANASAU KUWA ZINATAKIWA KULINDWA KWA GHARAMA ZOZOTE!!

    ReplyDelete
  34. Muandishi, Dola bilioni 350! Hish!

    ReplyDelete
  35. So watu wengi tumeongelea kuzidisha mizigo, lakini pia quality ina matter, Wachina wanazidisha mizigo kama hawana akili nzuri, kimsingi unaweza kulipa faini ya mwaka mzima halafu ukawa unazidisha mizigo utakavyo, lakini barabara zao ziko poa tuu. Kwa hiyo nahisi pia inabidi tuwe waangalifu sana kukagua kiwango cha barabara kabla ya kuanza kuitumia.Ubaya wetu ni kuwa tukiona barabara imeshajengwa basi tunafurahia bila ya kufikiria kama itadumu.

    ReplyDelete
  36. Jamani, hii hoja inakwenda vizuri lkn ni vyema tukajua barabara haiharibiki kwa sababu moja tu ya kubeba mizigo, kuna sababu nyingine nyingi. Ya kwanza ikiwa ujenzi chini ya kiwango. Shughuli za kibinadamu, kama mifugo, biashara pembeni mwa barabara na mambo kadha wa kadha. Mikondo ya maji na umri wa barabara.
    Kuna bara bara za mikocheni au senkenke au barabara ya namanga Arusha hizi bara bara zimeanza kuharibika hata kabla ya kukabidhiwa, lakini naomba ijulikane kuna mizani zaid ya Tisa kwa barabara za TZ, mtu atahonga kiasi gani na apate faida ? Kwa nn kusiwe na Mizani DSM safari zinapoanzia ? Kwa nn gari la anayezidisha uzani lisitafishwe pale uzani unapokwa beyond acceptable ? Je hii mizigo inayobeba haya malori inaishia TZ ? Kama inakwenda kwa nchi za jirani wao mbona barabara zao hazina shida? Na wao wana mizani pia. Naomba niwe muwazi issue yetu ni ujenzi chini ya viwango tunajenga hizi barabara chini ya viwango sana. Na barabara zingine umri wake umefika wa miaka 20. Angalia barabara zinazojengwa na mchina na mzungu tofauti ya ubora ni kubwa sana tafakari? Duniani kote malori na treni vinatoa huduma kwa pamoja angalia uingereza, SA, hata marekani. Issue hapa ni kiwango cha barabara. Barabara za mikocheni hazipitishi malori ziko hoi. Tunajengewa barabara za kubeba mikate ? Tuna angalia malori kwenye aspect moja basi tuangalie na mchango wake kiuchumi ? Kila ltr moja ya mafuta tsh 250 inakwenda kwenye ujenzi wa barabara bila malori kuleta na kutoa mizigo bandari yetu ingekuwa kama urembo tu. Fikiri ajira ambazo wanatoa na bandari inatoa ? Nadhani issue hapa tuwe wawazi watu wamejenga barabara chini ya viwango wanataka kuzilinda kwa kusema uongo kuhamishia lawama kwenye malori. Let's be fare na sote tutafakari kwa kina ukweli wa tatizo. Huwezi niambia mizani 9 mtu anapita bila kukamatwa ? Na si kweli magari ya tz yanabeba 56 hiyo ni maximum allowed on GVM. Yes sheria ya 1973 ifatwe na iheshimiwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...