Baadhi ya wananchi wa mji wa Mbeya wakiwa wabeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima wa Chadema, uliofanyika kwenye Uwanja wa Lwanda Nzovwe mjini Mbeya jana. 
Mbunge wa Mbozi Mashariki, Davi Silinde (Chadema), akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe mjini Mbeya jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akihutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, wakiondoka kwa shamrashamra, baada ya kuhutubia mkutano wa hadahara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwa amembeba mtoto Sheila Shukurani (3), kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara matika mji wa Makongorosi mkoani Mbeya jana.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, akiwahutubia wananchi wa mji wa Mbeya na vitongiji vyake katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe jana.
Picha na CHADEMA
The mdudu,huyu sugu toka awe mbunge sijui ashafanya nn cha maana kwa wananchi wake mnaoishi mbeya mjini hebu tupeni data maana isijekua akasahau ahadi zake zote alizotoa kwa wanachi wake,nauliza hivyo coz tunae wakwetu kule moro kwajina Afande Sele tunataka tumsimamishe ili autoe ulemzigo mzito usio bebeka
ReplyDeleteSwali zuri mdudu....Tanzania tulionayo sasa si ile ya zamani, mambo yanabadilika mno ni rahisi kufahamu ufanisi wa mtu kupitia anaowaongoza, mpaka kufikia unauliza swali bwana kakakuona,dhahiri kua Mbeya mjini ni shwari na Sugu moto chini.Bila shaka unazo taarifa zilizo zagaa za wanaoshutumiwa kua mizigo, si kwa chuki nisuala la uwajibikaji tu......
ReplyDeleteSugu zaidi music, barabara walau kajitahidi zimekarabatiwa ijapo zingine si kwa kiwango. Kichekesho ni bado Soko la Mwanjelwa limesimama kujengwa, hatujui hatma yake. Wafanyabiashara wa sido wanalia kwa barabara kujaa maji mpaka kwenye stoo zao za kuhifadhia bidhaa zao. Sijui tuseme nini kimefanyika na nini hakijafanyika. kajitahidi kiasi chake.
ReplyDelete