Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwasisitiza wanajumbe wa
chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma kuanzisha miradi ya
ufugaji nyuki ili kujiongezea kipato wakati akifungua mkutano mkuu wa
mwaka wa chama hiko uliofanyika jana mjini Dodoma.Kuanzisha.
Katibu wa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma Ndg. John
Mlabu akielezea changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu mkoani
Dodoma wakati akiwasilisha risala ya chama hicho kwa Mkuu wa mkoa Dodoma
Dr. Rehema Nchimbi (watatu) wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho
uliofanyika jana mjini Dodoma.
Baadhi ya wanachama wa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa
Dodoma wakisikiliza salamu za mkuu wa mkoa Dodoma (hayupo pichani)
wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika jana
mjini Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dr. Rehema Nchimbi na
wanachama wa chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA) Mkoa wa Dodoma mud
mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama
hiko uliofanyika jana mjini Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (
wapili kutoka kushoto waliochuchumaa) na wajnachama wa chama cha
walemavu Tanzania (CHAWATA) Mkoa wa Dodoma muda mfupi baada ya mkuu huyo
wa mkoa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hiko uliofanyika jana
mjini Dodoma.
=========== ======= =========
Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi ameziagiza wilaya zote za mkoa wa
Dodoma kuhakikisha zinatenga ardhi kwa ajili ya watu wenye ulemavu na
kusisitiza kuwa ardhi hiyo ni lazima iipimwe na kutolewa hatimiliki.
Aidha ametaka ardhi hiyo itakayotengwa kwenye kila wilaya itumike
kujengea ofisi za chama cha walemavu Tanzania Ngazi za wilaya na
kufanyia miradi ya uzalishaji illi kujipatia kipato.
Vilevile Dr. Nchimbi alitoa Rai kwa chama cha walemavu Tanzania CHAWATA mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanaanzisha miradi ya ufugaji nyuki ambayo wataifanyia kwenye ardhi watakazopatiwa na wilaya.
Dr. Nchimbi aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa CHAWATA mkoa wa Dodoma ambapo aliwatia moyo walemavu kwa kuwaeleza kuwa miradi ya ufugaji nyuki katika mkoa wa Dodoma imeonesha kufanya vizuri na soko zuri lipo ndani na nje ya Nchi. Aidha, Alieleza kuwa ufugaji nyuki hauhitaji fedha nyingi na wala haumuhitaji mtu kwenda kushinda kwenye mradi kila siku akifanya kazi badala yake nyuki wenyewe ndio wanafanya kazi ya uzalishaji, hivyo mradi huu wa ufugaji nyuki utakuwa wa manufaa sana kwa watu wenye ulemavu.
Aliahidi serikali kutoa msaada wa usimamizi na utaalamu katika miradi hiyo ya nyuki ambapo ameagiza maafisa ustawi wa jamii mkoa na wilaya kusimamia miradi itakayoanzishwa na maafisa nyuki wa wilaya wahakikishe wanahudumia miradi hiyo upande wa utaalamu na amezitaka halmashauri za wilaya wahakikishe wanaweka mkundombinu ya usimamizi ikiwa ni pamoja na kugharamia gharama za wasimamizi wa hiyo miradi.Hiyo
Dr. Nchimbi alimaliza kwa kuwaasa CHAWATA kuwa mapato ya miradi hiyo ya nyuki yatumike kugharamia gharama za uendeshaji wa shughuli za CHAWATA ili walemavu waendeshe shughuli zao bila kutegemea kuomba misaada, vilevile mapato hayo yanaweza kutumika miradi mingine zaidi ya uzalishaji na hivyo kuwanyanua walemavu mkoaniDodoma.
Nae katibu wa CHAWATA mkoa wa Dodoma Ndg. John Mlabu akiwasilisha taarifa ya chama chake Ameeleza kuwa wanakumbana na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu vyumba vya ofisi za wilayani, halmashauri nyingi hazitengi bajeti kwa ajili ya walemavu, walemavu kutotengewa maeneo ya biashara kwenye maeneo yanayoainishwa kufanyia biashara na gharama za visaidizi mwendo (magongo, wheelchairs na tricycle) kuwa juu.
Nyingine ni bei kubwa za viwanja vinavyouzwa na mamlaka ya uendelezaji makao makuu CDA ambapo walemavu hawawezi kuzimudu na vilevile majengo mengi hasa maghorofa na baadhi ya ofisi nyeti hayajazingatia miundombinu ya watumiaji walemavu.
(HABARI NA PICHA NA JEREMIA MWAKYOMA - OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA)

Nyuki wakikasirika, ni wakali kweli. Nyuki waliwahi nifukuza na kuningata miaka mingi iliyopita. Sijawasogelea tena.
ReplyDelete