BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni Juni 1, 2014 kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana socil hall wa Morogoro.
Cheka amesema amejiandaa kupigana kawa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni bondia huoyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Francis Cheka ambaye alikuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe. Amesema yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo.
Mpambano huo utakaosimamiwa na TPBO utasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakaevaana na Sadiki Yusufu wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu.
Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic Miyeyusho, Japhet Kaseba Vs Thomas Mashali, Floyd Mayweathar na Manny Paquaio, Saul 'canelo' Alverez, Mike Tyson, Mohamed Ali, Felix Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi.
 DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa zawadi kwa mabondia na Kocha Super D ambaye ameahaidi kutoa, Gum sheets, Clip Bandeji, DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa hali ya juu wa kutupiana masumbwi
Cosmas Cheka (kushoto) baada ya kutangaza mpambano wake na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana socil hall  wa Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...