Watuhumiwa wawili katika tukio la ujambazi lililotokea Mchana wa leo eneo la Darajani Jua Kali,Zanzibar wametiwa mbaroni baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi wenye wakati walipokuwa wakiwakimbia Polisi.
Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walikuwa watatu na walitaka kuiba katika maduka na mawakala wa huduma za pesa yaliyopo eneo la Mnazi Mmoja. Baada ya kushtukiwa walikimbia na kufukuzana na Polisi hadi katika maeneo ya Darajani ndipo wananchi kwa kushirikiana na polisi wakawadhibiti na kuwakamata. Hata hivyo mmoja wao alifanikiwa kutoroka na hadi sasa anasakwa na jeshi la polisi.
Pia wapo baadhi ya wananchi wamelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kupatwa na mshtuko kutokana na risasi zilizokuwa zikipigwa hewani na mmoja aligongwa na gari la watuhumiwa hao wakati wa kukimbizana na askari.
Mmoja kati ya waliokamatwa na aliepata kipigo kikali anadaiwa kuwa ni jambazi sugu ambae alikuwa akitafutwa na Polisi kwa kipindi kirefu.

Watuhumiwa hao walikuwa na gari aina ya Toyota Noah lenye namba za Usajili T 736 CGT na walikamatwa baada ya gari lao hilo kushindwa kuendelea na safari baada ya kuingia kwenye njia ambayo hairuhusiwi.
Askari Polisi pamoja na raia waliokuwepo eneo la tukio wakiwa wamemzunguka mmoja wa watuhumiwa hao wa ujambazi baada ya kumtia mbaroni mchana wa leo,katika eneo la darajani Jua Kali,Zanzibar.
mmoja wa watuhumiwa hao akiwa chini ya ulinzi ndani ya Gari la polisi.
Sijafurahi kwakuwaona wanapelekwa hospitali inavyotakikana kupelekwa kufukiwamoja kwa moja ili liwe funzo kwa wengine
ReplyDeleteKweli ulivyosema ili iwe fundisho kwa wengine. Dar jana mapolisi wetu wamepunguza majambazi wawili. Polisi endelezeni mwendo huu miji itakuwa shwari na mawakala watafanya kazi bila kuhatarisha maisha yao. Nasi wananchi kufurahia huduma za uhakika kwani bado miamala ya pesa taslmu haitaisha leo. Kubadilika inachukua muda.
DeleteThe stupidity and backwardness of the society and some people still abetting mob justice is just beyond me. A few days ago there was a video where for the first time I saw some emotionally intelligent people intervening the beating of a purported thief. Those who were in the frontline could not even say what that kid had stolen and the beaten up guy was set free. Mob justice can affect anyone even YOU who are abetting this primitive nonsense of taking law to one`s own hands.
ReplyDeleteWewe ulosema haifai kuchukua hatua mikononi , ngoja haya majambazi wakuingile wewe na silaha , then uwakamate uwapeleke polisi
ReplyDeleteHao walikuwa weshaandaliwa matairi ya gari na wananchi wenye hasira kali (kwa mujibu wa picha zilizokuwa zikisambaa kwa njia ya simu) na ilikuwa tayari kuwabanika wazima wazima, salama yao ndio huko kupelekwa hospitali, labda uamuzi huo ili waweze kupona na kuwadhibiti zaidi ili wawataje na hao wenzao na mtandao wao mzima wa kijambazi kw jumla, huenda itasaidia somehow, kuliko kuwafukia moja kwa moja, ambapo tatizo bado litakuwa halijatatulika.
ReplyDelete3rd anonymous, there was a clean sheet evidence showing that those guys were bandits and that there was no need to send send them before the corruptive magistrates where they could escape conviction for what would claimed to be lack of proof beyond reasonable doubt!!!! For your information even, even the 'civilized' nation known as the United States does the same, refer the cases at Guantanamo in Cuba.
ReplyDeleteSo, in most cases mob justice use to be the right solution.