Katika
gazeti la Tanzania Daima ukurasa wa 5, toleo namba 4070 la tarehe 25 Januari,
2016, lilichapisha habari yenye kichwa cha habari Polisi “waisoma” namba. Sehemu
ya taarifa hiyo inaeleza kuwa askari Polisi hivi sasa wanatakiwa kujilipia
gharama za umeme.
Jeshi la Polisi nchini, linakanusha vikali taarifa
hiyo kwamba siyo sahihi. Ukweli ni kwamba askari polisi wote makambini wanalipiwa
umeme na serikali, ikiwemo wale ambao
nyumba zao zimefungiwa luku kama njia ya kuboresha huduma na matumizi sahihi ya
umeme. Baada ya askari kununua umeme hutakiwa kuwasilisha stakabadhi ya malipo
ya umeme kwa ajili ya kurudishiwa kiasi cha fedha walichonunulia umeme kila
mwisho wa mwezi.
Aidha, habari iliyochapishwa na Tanzania Daima
ililenga kupotosha umma na mwandishi wa habari hiyo hakutafuta ufafanuzi kutoka
kwenye mamlaka husika.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini, linamtaka
mhariri wa gazeti la Tanzania Daima na waandishi wake wa habari kuwa makini na
habari wanazoziandika hasusani taarifa zinazohusu vyombo vya ulinzi na usalama
ili kuepuka madhara ya kiusalama yanayoweza kutokea kutokana na habari
wanazozitoa zisizo na usahihi.
Imetolewa na:-
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...