Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa kampuni ya Gezhouba kutoka China kuhusu masuala ya uwekezaji. Kushoto ni kiongozi wa msafara huo Mhandisi Hu pend.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa kampuni ya Gezhouba kutoka China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Shell Deepwater Tanzania BV Alex Knope walipokutana leo ofisini kwake Ikulu kwa ajili ya kumsalimia.
Vizuri nchi yetu yaweka kipaumbele kwa wawekezaji, na haswa wachina wako bongo wanaishi Kama wabongo na kuwa kama wabongo mfano mzuri mpaka wamachinga sku hizi sio wabongo tu mpaka wachina mpaka kwenye kuuza njugu. Sasa wanafanana pia na wabongo, Kama tunavyoona picha ya kwanza huyo boss sio mwembamba kama tulivyozoea wachina kwa kawaida ni wembamba, haya na ukija kwenye picha ya pili ya pamoja na makamu wa Rais huyo mama wa kichina mnene kama wanavyotakiwa wakina mama wa kiafrika. Vizuri sana tena sana na tena inapendeza sana unapoenda kuishi kwenye nchi ya wenzio na wewe ukifanana na wenye nchi kwa kila jambo inapendeza, tunauhakika hawa wanapenda hata vyakula vyetu hususani ugali na maharage.
ReplyDeleteSAFI SANA WAWEKEZAJI WAZIDI KUJA KWA KASI. LAKINI KUWA MAKINI WENGI WALISHAINGIA HAWANA VIBALI MAALUMU VYA KUISHI. NI MATEGEMEO YETU PIA UTEUZI WA RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KUMRUDISHA WAZIRI SOSPETER MUHONGO KWENYE WIZARA YA NISHATI NA MADINI NI WA BUSARA KWAMANA ALIIMUDU VYEMA WIZARA HII NA ASIDHARAU WAZAWA WATANZANIA AWAPE KIPAUMBELE ILI WAWE BEGAKWABEGA NA WAWEKEZAJI KUNGIA NCHINI KUWEKEZA KIKAMILIFU. INAWEZEKANA KABISA. HAPA KAZI TUU
ReplyDelete