Rais Mteule wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akitia saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu baadanya kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nadhani 'Kuteuwa' na kuchaguwa ni maneno mawili ya kiswahili yaliyo tofauti na yenye maana mbili tofauti. Inaposomeka Rais Mteule wa Zanzibar....ukweli halisi kimaana, huyo hakuteuliwa, bali alipigiwa kura halali kabisa na wananchi wa Zanzibar na ndiye aliyeibuka mshindi kwa kuongoza kwa asilimia kubwa katika matokeo ya kinyang'anyiro hicho cha Urais wa Zanzibar. Hivyo tumpe hadhi yake inayostahili sio kusema Rais Mteule...neno mteule hapo linaleta mushkel na kupotosha kimaana. Mh. Dk. Ali Mohamed Shein, alikuwa 'ELECTED' (Kachaguliw) na wananchi wa Zanzibar kwa kura zao na sio kawa 'APPOINTED' (kateuliwa). Maana unapomteuwa mtu ina maana hakuna maamuzi ya walio wengi for some reasons. Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza fungua macho.......mimi nakubariana na mwandishi mia kwa mia.....kalaghabao, unatoa lecture ya kiswahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...