Kufuatia kifo cha mwana wa chuoni mkubwa nchini Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla Sheikh Muhammad ibnu Abii Bakaril Burhaan ambae alikuwa ni mkuu wa chuo cha Shamsul Maarif kilichopo mkoani Tanga, imeonekana ni busara kufanya dua ya kumuomba Allah amfanyie wepesi ktk safari yake.

Fikra imekuja sio tuu kwa kukiri mchango wake mkubwa kwa wa- Islam na u- Islam lakin kwa wanadamu kwa ujumla. Dua imepangwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 19/03/2016 saa nane mchana maeneo ya Barking, East London ukumbi utatajwa baadae.

Masheikh wengi na wadau mbali mbali wanategemea kuhudhuria na tunawaomba wote watakao jaaliwa tushirikiane ili kufanikisha jambo hili tukufu.

Kwa mawasiliano zaidi na yote yanayo husu shughuli nzima wasiliana kwa namba zifuatazo: 07986142485 au 07904962787 au 07453530218. Mahudhurio yako ndio mafanikio ya shughuli hii. Mnakaribishwa,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mwenyeez Mungu amrehemu, amughufiriye kwa yote na kumjaaliya makazi mema peponi - Amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...