Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Jeddah, Saudi Arabia, Suleiman Saleh amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS, Saleh Said Bakhatab,  ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa mifugo nchini Saudi Arabia, Bw. Saleh alimkaribisha Bw. Bakhatab ofisi kwake Jeddah, ambapo alipata maelezo ya kina kutoka kwa mgeni wake huyo kuhusiana na utayari wake wa kununua na kusafirisha mifugo mbali mbali wakiwemo ng'ombe, kondoo na mbuzi kwa ajili ya soko la Saudi Arabia.

Bakhatab alibainisha kwamba kwa miaka 25 amekuwa akinunua kondoo, mbuzi na ng'ombe kutoka Sudan, Ethiopia, Somalia, Australia, Romania na Uruguay na utafiti wake umeonyesha kwamba Tanzania ina mifugo yenye ladha nzuri kutokana na aina ya malisho bora, Kwa mantiki hiyo, Bakhatab alimuomba Konseli Mkuu kumuandalia miadi na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye dhamana ya sekta hiyo ili kukamilisha azma yake hiyo.

Aidha Bakhatab alimweleza Saleh kwamba kuna mambo ya msingi ambayo katika kufanikisha biashara hiyo ni vyema yakaandaliwa ili biashara ifanyike kisasa na kwa ufanisi mkubwa. Mambo hayo ni pamoja na kuandaliwa utaratibu endelevu wa kupatikana kwa mifugo hiyo kulingana na mahitaji ya soko la Saudi Arabia, Pili, kuandaa mazingira elimishi kwa wafanyakazi wa bandari na viwanja vya ndege ili wawe na ufahamu wa kina kuhudumia mifugo inayosafirishwa ambapo alionyesha utayari wake kusaidia katika kuleta video za mafunzo hayo.

Pia alishauri kuandaliwa eneo mahususi la Karantini kwa mujibu wa taratibu za kiafya za kimataifa ambapo mifugo inahifadhiwa na kupata huduma ya uchunguzi sahihi kabla ya kusafirishwa. Mwisho, Khatab alipendekeza mkutano baina yake na viongozi wa Wizara husika nchini Tanzania ili kuweka mikakati ya haraka ya kufanyika kwa biashara hiyo.

Kwa upande wake Suleiman Saleh alimhakikishia Bakhatab kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli imeanza kazi kwa kasi ya aina yake kwa kujenga mazingira rafiki na yenye ufanisi wa hali ya juu na kumuahidi kwamba atawasiliana na viongozi wa Wizara ya Kilimo na Mifugo ili wampokee atakaposafri kutembelea Tanzania hivi karibuni.
Konseli Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jeddah,Saudi Arabia, Suleiman Saleh, akimkaribisha ofisini kwake Mmiliki wa Kampuni ya SALEH SAEED ESTABLISHMENT FOR CONTRACTING AND CATTLE IMPORTS ya Saudi Arabia, Saleh Saeed Bakhatab, tayari kwa mazungumzo.
Bw. Suleiman Saleh akiendelea na mazungumzo na Bw.Bakhatab.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu Mzee ameondoka Washington, DC?

    ReplyDelete
  2. Uhashangaa, wafanya biashara hawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...