Na Raymond Mushumbusi, MAELEZO
Serikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.
“ Napenda kuwambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema Kidata.
Kamishna Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya.
Kamishna huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo zimekuwa kero na hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri zote nchini.
Hilo ni jambo la msingi. Kama mmesoma somo la hisabati mtashindwaje kufanya mchanganuo mzuri wa kulipa kodi. Kila mtu ni lazima alipe kodi. Lakini vile vile ni vigumu kuweka kodi nyingi kwa mtu mmoja. Punguzeni msululu wa kodi. Watu wengi zaidi watalipa kodi. Punguzeni kodi kwenye vifaa vya ujenzi na hospitali. Vitu hivi vitachochea shughuli za ujenzi na uchumi utaluwa zaidi. Wekeni mikakati ya kumfanya kila mtu alipe kodi. Hata kama nk mia tano. Lakini lazima walipe kodi. Hongera kwa hilo.
ReplyDeleteTRA lazima waunde kikosi cha Economy Intelligence Unit kwa ajili ya kuchakata vyanzo vya mapato toka katika ujenzi,ICT,Afya,Nuclear,Kilimo,Uvuvi,Utalii ,Transport,gas,fuel,nk hawa wanatakiwa kuwa weledi wa kuishauri TRAwhat we need to do ili kupata mapato mtu asipodai risti itungwe sharia ya kufungwa mwaka ni big sabotage,halafu wakati Prof Mbilinyi anafanya utafiti wa kuunda TRA alishauri iundwe Mamlaka ya Matumizi Tanzania ili hii iwe mizania ya kuangalia matumizi yanaenda kama yalivyopangwa .Vijana washiriki kuunda uchumi wa nchi yao naumia kuona Tanzania tuko nyuma kwenye e commerce kuuza vitu vyetu nje ili tupate fedha za kigeni.
ReplyDeleteTRA ifanye kazi kwa kushirikiana na taasisi kama TFDA,TBS<UNIVESITIES,EMBASSIES,TECHNICAL SCHOOLS NA BANKS kuhakikisha mapato yanapatikana .Na TRA waintroduce super computer ambazo ni rahisi kuhusianisha taarifa za wateja yaani mtu kanunua nguo Hong Kong amelipa banks ya NMB taarifa zake zinaenda TRA na jina lake ,wakati akiingiza mzigo inalinganisha na mzigo na pesa zilizopelekwa nje TFDA akikagua tarifa anapeleka kwenye super computer ya TRA TBS akikagua bidhaa anatuma taarifa TRA tunamiss coordination ya Taarifa za bidhaa mpaka tunakosa taxi base wakwepa kodi ni wengi taarifa zote ziwe processed na TRA kila taarifa iwe na link