Kituo cha EFM redio kwa mara nyingine tena kimeibuka na shindano lake la shika ndinga kwa mashabiki wake wa jiji la Dar na Pwani. Pamoja na kufanyika kwa shindano hilo lililozua msisimko mkubwa miongoni mwa wilaya ya Temeke,EFM Radiao pia waliwatangaza watangazaji wao Wapya watatu waliokuwa Clouds FM,Watangazaji hao ni Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando.Shindano hilo Kwa mwaka huu ,limezinduliwa rasmi jana April 9/2016 kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke  jijini Dar.

Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo alisema kuwa shindano hilo litaendelea pia kwa wilaya ya Ilala, Kinondoni, Bagamoyo, na Kibaha na hatimae kilele chake kufanyika katika uwanja wa Sinza TP.


Sebo alisema kuwa Shindano hilo litaanza na washiriki 60 kwenye kila wilaya na washiriki 10 kati yao wanawake watano na wanaume watano ambao wataingia kwenye fainali ya kujinyakulia gari ambao wamepata nafasi ya kushiriki kwa njia ya kupiga simu na kujibu kiufasaha swali husika ili kupata nafasi ya kushiriki shindano la shika ndinga.
Alisema kuwa shindano hilo mwaka huu limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali.Lengo ni kuwawezesha wasikilizaji wake kwa namna moja ama nyingine katika kuongeza na kukuza kipato kitakacho changia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, DenisSebo akiwatambulisha watangazaji wapya wa kituo cha redio cha Efm,Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando kwa wananchi jana katika shindano la shika ndinga kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
Watangazani wapya Paul James na Gerald Hando na ,Abel Onesmo akielekea jukwaani kutangazwa rasmi kwa wakazi wa Temeke,jijini Dar.
Watu wa huduma ya kwanza wakiwahudumia washiriki wa Shindano hilo waliokuwa wamezimia kutokana na mshtuko alioupata kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Salehe Maga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo.
Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Philipina Mshanga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo , na kuwaomba wakina wanawake wajitokeze kwa wingi kwenye mashindano hayo.
Ndinga na pikipiki zikiwa juu ya jukwaa kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Siyo mnakariri tu kuinua miguu juu ili ku-improve circulation, kama mgonjwa anapumua bila noma, basi muweke kwenye recovery position aka left lateral position, hapo huyo binti (aliyezirai) alipo AKITAPIKA, basi atakuwa choked na matapishi yake ( You had a patent airway and have just lost it). Halafu huyu NJEMBA aliyezimia naye ni "JIPU" tu, toka lini mtu aliyezirai anaweza kunyanyua na ku-uweka mguu wake juu hewani? (angalia mguu wake wa kulia).
    Kumbukeni wenzangu wa afya, the ABCDE of an acutely ill or of an unconscious patient.
    A- airway
    B- breathing
    C- circulation
    D- disability/diagnosis
    E- exposure/examination

    Dr G. Bitozi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...