Marehemu Dkt. Aaron Daudi Chiduo
Tarehe 23 May 1933 – 13 April 2007
Baba yetu mpendwa, Masaa, Siku, Wiki, Miezi na sasa ni miaka 9 tangu Mungu wetu mwenye wingi wa rehema na upendo alipodhihirisha utukufu na mapenzi yake makubwa kwako hadi akaamua kukuchukua alfajiri ya siku ya Ijumaa terehe 13/04/2007.
Huzuni na majonzi bado vimebaki kuwa ni sehemu ya maisha yetu katika familia lakini tunalo lile tumaini la Neno la Mungu kuwa siku moja tutaufikia ule ufufuo wa milele ndani ya Kristo pamoja. Matendo yako mema yamebaki kuwa lulu na mwanga uiangaziayo familia yetu.
Maisha yako ya upendo, unyenyekevu, uadilifu, utu wema na bidii katika kazi ndiyo dira inayotuongoza: mke wako Mama Ahilai, watoto wako Sydney, Sarah, Oripa, Geoffrey, Rodney, wakwe zako Pascal, Joel, Eunice na Salome pamoja na wajukuu zako Dennis, Karen, David, Samantha, Jovin na Daniel. Tutakukumbuka sana na kukulilia siku zote kwa kukukosa katika mengi.
Dada zako Anna, Esther, Harriet, Monica na Magdalena, Mdogo wako Nicholas na familia zao na ndugu wengine wote wa koo za Chiduo, Chitemo, Chigongo, Mheta, na Msele nao pia wanakukumbuka sana. Kwetu sote imebaki kumbukumbu ni jinsi gani ulikuwa mhimili wa familia na ukoo mzima kwa ujumla.
Rafiki zako, Madaktari wenzako, Wanasiasia wenzio na wengineo bado wanakumbuka bidii yako na mchango wako mkubwa ulioutoa katika kulitumikia Taifa hili. Bado wanazungumzia hulka yako ya uaminifu, uadilifu, unyenyekevu na kupenda haki viliyokujengea heshima kubwa miongoni mwa jamii.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe.
1 Wathesalonike 4:13-14 Neno: Bibilia Takatifu
13 Ndugu wapendwa, hatupendi mkose kujua kuhusu wale wanaokufa, au mhuzunike kama watu wasiokuwa na tumaini. 14 Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, kwa hiyo tunaamini kwamba Mungu atawainua wale waliokufa pamoja na Kristo wakiwa ndani yake.
This man was saintly
ReplyDeleteGod bless his soul
Dr Ibrahim Manthy
Hawa ndio wabunge, mawaziri waadilifu of all time! amefariki maskini huyu Mzee aliweka uzalendo mbele! mke wake alikuwa Nurse pale arnatoglo!
ReplyDeleteInna LiLLAH wa Inna Ilaihi Raajiuun !
HAta mimi namkumbuka Mzee Chiduo!