Na Mwandishi
Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa
nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 175 ambao wametia sahihi kuhusu Makubaliano ya Mabadiliko ya Tabia nchi (
Paris Agreement) yaliyofikiwa katika mkutano uliofanyika Jijini Paris- Ufaransa mwezi Desemba 2015.
Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa ndiyo aliyepewa dhamana ya kutia sahihi makubaliano
hayo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika hafla
ya kihistoria na ya aina yake
iliyofanyika siku ya Ijumaa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema haijawahi kutokea Mkataba
au Makubaliano ya Kimataifa kutiwa sahihi na mataifa mengi
katika siku ya kwanza kama ilivyokuwa
kwa Makubaliano ya Paris.
Mataifa makubwa na
ambayo yanachangia katika utoaji wa gesi
chafu ya ukaa( carbon dioxide) kama Marekani, China, Urusi, India , Ufaranza na
mengineyo nayo yameweka sahihi zao.
Aidha, Getrude Clement(16) kutoka Mwanza -Tanzania alizungumza katika hafla hiyo akiwakilisha
ujumbe kutoka kwa vijana wenzie duniani kote.
Getrude alizungumza kwa umahiri wa hali ya juu, akianisha
mambo kadha wa kadhaa ambayo vijana wa kizazi chake na kijacho wangependa kuona
kizazi cha sasa kikiyatekeleza kupitia Makubaliano hayo ya Paris ili nao
waje kuishi na kuifaidi Sayari
Dunia.
“Mabibi na Mabwana sasa nina mkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa azungumze nanyi. Katibu Mkuu Karibu” akasema Getrude kauli
iliyoufanya ukumbu mzima kumpigia makofi
Akizungumza baada ya
kutia sahihi, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na mambo mengine
amesema, kwa Tanzania kutua
sahihi Makubaliano nayo ni hatua
moja kwenda hatua ya pili ya kuridhia.
Akasema, Tanzania inaserikali
makini na Bunge makini ambalo kwayo limeweka mbele na kutilia mkazo suala
la utunzaji wa mazingira na kwa sababu hiyo hapana shaka haitachukua
muda mrefu wa kuridhia Makubaliaano
hayo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
![]() |
| Getrude Clement(16) kutoka Mwanza -Tanzania alizungumza katika hafla hiyo akiwakilisha ujumbe kutoka kwa vijana wenzie duniani kote. |
Getrude akizungumza kwa umahiri wa hali ya juu, akianisha mambo kadha wa kadhaa ambayo vijana wa kizazi chake na kijacho wangependa kuona kizazi cha sasa kikiyatekeleza kupitia Makubaliano hayo ya Paris ili nao waje kuishi na kuifaidi Sayari Dunia.







Safi sana. Tunamwomba Rais amwite kijana huyu Ikulu na kumpa zawadi. Ametuwakilisha vizuri sana.Good things are happening in Tanzania.
ReplyDeleteAmetuwakilisha vizuri sana. We are proud of you.
ReplyDelete