Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni   miongoni mwa  nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 175 ambao wametia sahihi    kuhusu   Makubaliano ya Mabadiliko ya Tabia nchi ( Paris Agreement) yaliyofikiwa katika mkutano uliofanyika  Jijini Paris- Ufaransa mwezi Desemba 2015.
Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ndiyo aliyepewa dhamana ya kutia sahihi makubaliano hayo kwa niaba ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika hafla ya  kihistoria na ya aina yake iliyofanyika siku ya Ijumaa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban  Ki Moon, amesema haijawahi kutokea Mkataba au  Makubaliano ya  Kimataifa kutiwa sahihi na mataifa mengi katika siku ya kwanza  kama  ilivyokuwa  kwa Makubaliano ya Paris.
Mataifa makubwa  na ambayo yanachangia katika utoaji wa  gesi chafu ya ukaa( carbon dioxide) kama Marekani, China, Urusi, India , Ufaranza na mengineyo nayo yameweka sahihi zao.
Aidha, Getrude Clement(16)  kutoka  Mwanza -Tanzania  alizungumza katika hafla hiyo akiwakilisha ujumbe kutoka kwa vijana wenzie duniani kote.
Getrude alizungumza kwa umahiri wa hali ya juu, akianisha mambo kadha wa kadhaa ambayo vijana wa kizazi chake na kijacho wangependa kuona kizazi cha sasa kikiyatekeleza kupitia Makubaliano hayo ya Paris ili  nao  waje kuishi na kuifaidi  Sayari Dunia.
“Mabibi na Mabwana sasa nina mkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azungumze nanyi. Katibu Mkuu Karibu” akasema Getrude kauli iliyoufanya ukumbu mzima kumpigia makofi
Akizungumza baada ya  kutia sahihi, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na  mambo mengine  amesema,  kwa Tanzania kutua sahihi Makubaliano nayo ni  hatua moja  kwenda hatua ya pili ya kuridhia.
Akasema, Tanzania inaserikali  makini na Bunge makini ambalo kwayo limeweka mbele na kutilia mkazo   suala  la utunzaji wa mazingira na kwa sababu hiyo hapana shaka haitachukua muda mrefu wa kuridhia Makubaliaano  hayo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
 Getrude Clement(16)  kutoka  Mwanza -Tanzania  alizungumza katika hafla hiyo akiwakilisha ujumbe kutoka kwa vijana wenzie duniani kote.
 Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akitia  sahihi makubaliano hayo kwa niaba ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika hafla ya  kihistoria na ya aina yake iliyofanyika siku ya Ijumaa.
 Getrude Clement akiwa na ujumba wa Tanzania  uliongozwa na  Balozi Tuvako Manongi wakati wa utiaji sahihi wa Makubaliano ya Tabia nchi. ( Getrude) ni mwanaharakati wa mazingira kwa kushirikina na UNICEF. 
 Getrude akizungumza kwa umahiri wa hali ya juu, akianisha mambo kadha wa kadhaa ambayo vijana wa kizazi chake na kijacho wangependa kuona kizazi cha sasa kikiyatekeleza kupitia Makubaliano hayo ya Paris ili  nao  waje kuishi na kuifaidi  Sayari Dunia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliozungumza kabla ya utiaji sahihi wa  Makubaliano  ya Paris kutoka  kushoto ni  Hindou Oumarou Ibrah(Chad) aliwasilisha ujumbe wa asasi za kiraia,  Bw Leonardo Di Caprio mcheza senema maarufu na Mjumbe Maalum kuhusu amani , na  Getrude Clement ( Tanzania) aliyezungumza kwa niaba ya vijana. Msikilize Getrude akiongea umoja wa mataifa mbele ya viongozi wa dunia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safi sana. Tunamwomba Rais amwite kijana huyu Ikulu na kumpa zawadi. Ametuwakilisha vizuri sana.Good things are happening in Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Ametuwakilisha vizuri sana. We are proud of you.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...