WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa mbao kutoka katika mashamba nane ya miti ya kupandwa yanayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Serikali  kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inamiliki mashamba ya miti ya kupandwa 18, na kati ya hayo uvunaji umekuwa ukifanyika katika mashamba nane ambayo ni Sao Hill (Mufindi), Buhindi (Sengerema), Meru/Usa (Arumeru), West Kilimanjaro (Hai), Shume (Lushoto), North Kilimanjaro (Rombo), Kiwira (Rungwe) na Kawetire (Mbeya Vijijini).

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Julai 8, 2016) na kufafanua kwamba usitishaji huo unalenga kutathmini taratibu, kanuni na vigezo sahihi vinavyotakiwa kutumika katika kugawa malighafi kutoka kwenye mashamba hayo.

Amesema wadau wote wa viwanda vinavyojikita katika malighafi ya misitu na hususan wamiliki wa viwanda vya kupasua mbao wanashauriwa kuwa watulivu wakati utaratibu huu ukifanyiwa mapitio na umma utatangaziwa rasmi pindi uboreshaji huo utakapokamilika.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

IJUMAA, JULAI 8, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...