Na Dotto Mwaibale, Kibaha

KUNDI la WathAssp la Afya yangu limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 900,000 kwa ajili ya kujifungulia wajawazito kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi mkoani Pwani.

Vifaa hivyo vilivyopokelewa na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa vilikabidhiwa katika kituo hicho huku tukio hilo likishuhudiwa na Diwani wa Mlandizi, Euphrasia Kadala na wauguzi wa hospitali hiyo.

Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Mbunge Jumaa alisema msaada huo umefika kwa wakati muafaka na utasaidia wajawazito katika hospitali hiyo.

"Msaada huu tulioupokea leo hii utawasaidia wajawazito wanaofika kujifungua katika kituo hiki tuna washukuru sana" alisema Jumaa.

Alisema yeye yupo katika makundi ya WathAssap 36 lakini hajawahi kuona yakitoa msaada kwa jamii kama lililofanya kundi hilo la AFYA YANGU ambapo alitoa ushauri kwa makundi mengine kuiga mfano huo.

Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale alisema kama kundi waliguswa na kusukumwa kusaidia katika eneo hilo kufuatia mafunzo ya afya wanayopata kutoka kwa wataalamu wa afya ambao ni wanachama katika kundi hilo.

"Katika kundi letu tuna madaktari ambao hutupa mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya afya ambapo kupitia mafunzo hayo tukasukumwa kuchangishana na kusaidiwa na wadau wengine na kuona tufanye hiki tulichokifanya" alisema Lulale.
 Msimamizi Mkuu wa Kundi la WhatsAPP la AFYA YANGU, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (kushoto), akimkabidhi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, vifaa vya kujifungulia wajawazito vilivyotolewa na kundi hilo kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi jana. Kulia ni Mwanachama wa kundi hilo, Mudeme Elly.
 Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (katikati), akitoa maelezo wakati akikabidhi msaada huo.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Mlandizi, Sahib Katyene, akitoa maelezo wakati akipokea msaada huo.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, akizungumza wakati akipokea msaada huo.
 Vifaa hivyo vikipokelewa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...