NA ELISA SHUNDA, MUHORO-RUFIJI
WANANCHI na Wadau mbalimbali waombwa kushikamana kwa pamoja na kuondoa tofauti ya itikadi za kivyama na kushiriki kwa pamoja kuisaidia serikali katika ukuzaji wa maendeleo ya jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Mazingira na sekta ya Miundombinu.
 
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mh. Haji Haidari kwenye harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote iliyopo Kata ya Muhoro wilayani Rufiji ambapo alisema kuwa hadi jumuiya hiyo ya wazazi kufikia uamuzi wa kufanya harambee ya ujenzi wa shule hiyo ni kutokana na umbali uliopo wa Kilometa 12 kutoka kwenye Kijiji cha Nyandote na Shule ya Msingi Muhoro hali iliyosababisha wanafunzi walio wengi kutomaliza shule kulingana na changamoto mbalimbali ikiwemo kubakwa na kulawitiwa njiani na watu waovu,mimba,njaa na umbali wa shule ilipo.

“Nawapongeza wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama na jumuiya zake kwa kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha tunafanikisha harambee hii ya ujenzi wa shule ya msingi ya Nyandote ambapo si kwa faida ya watoto wa wanachama wa CCM peke yake bali ni watoto wa jamii nzima nawashukuru sana kwa mlivyojito.

“Kwa kujitolea kwenu huku shule ya msingi Nyandote ikikamilika tutakuwa tumewasaidia wanafunzi 430 kuanza masomo yao lakini pia tutakuwa tumewaepusha wanafunzi hao na kutembea umbali mrefu wa Kilometa 12 kuja shuleni Muhoro pia tutawaepusha na vishawishi mbalimbali za njiani,tutawaokoa na kubakwa na kulawitiwa njiani na watu waovu” Alisema Mh.Haidari
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji (katikati) akikabidhi mifuko 230 pamoja na fedha taslimu Sh. 650,000 kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote iliyopo Kata ya Muhoro Wilayani humo jana. Picha zote na Elisa Shunda. 
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Muhuro,Mary Msigwa (katikati) akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji (kulia) kuhusu kupokea mifuko 230 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote na amekabidhiwa Sh. 440000 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo kwenye shule ya Msingi ya Muhuro iliyopo wilayani Rufiji.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji akizungumza na wananchi kuhusu kupokea Sh.200,000 na Mifuko ya Simenti 100 kutoka kwa Mwenyekiti wa Uchumi Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Rufiji,Juma Salum Mpendu “Chogo” kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la Nyandote
Wazee wakifuatilia kwa umakini mkubwa mkutano huo wa harambee kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo kwenye shule ya Msingi ya Muhuro iliyopo wilayani Rufiji .
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani, Jackson Kituka akizungumza kwenye mkutano huo wa harambee.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...