Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiongozwa na Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati, wamekagua mradi wa umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika wilaya mbalimbali mkoani Tanga na kuzindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo, wilayani Korogwe.
Mhandisi Msembele, ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu katika uzinduzi huo, alisema kuwa, kuzinduliwa kwa huduma ya umeme katika Kijiji hicho kumewezesha wananchi zaidi ya 63 kuunganishwa na huduma ya umeme huku wateja 180 tayari wameshalipia huduma hiyo.
" Niwapongeze wananchi wa Kijiji hiki cha Bagamoyo kwa kuchangamkia huduma ya umeme, lakini niwakumbushe kuwa inapaswa kutumia umeme kwa ajili ya kufanya shughuli za kiuchumi kama kufunga mashine za kusaga nafaka na si kuwasha taa peke yake, " alisema Mhandisi Msembele.
Wataalam wengine walioambatana na Mhandisi Msembele ni Afisa Upimaji kutoka REA, Hussein Shamdas, Meneja wa TANESCO mkoa wa Tanga, Eng. Cecilia Msangi na Meneja wa TANESCO, wilaya ya Korogwe, Julius Nyamarungu.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakikagua transfoma zitakazotumika kusambaza umeme vijijini katika Wilaya ya Korogwe. Kushoto ni Hussein Shamdas kutoka REA na katikati ni Yusuph Msembele.
Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati (wa Tatu kulia) akikata utepe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo wilayani Korogwe mkoa wa Tanga. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka TANESCO, REA na wawakilishi wa wananchi.
Mhandisi Yusuph Msembele kutoka Wizara ya Nishati akibonyeza kitufe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Bagamoyo wilayani Korogwe mkoa wa Tanga. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka TANESCO, REA na wawakilishi wa wananchi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...