*Yaagiza Kaimu Mkurugenzi wa
Bodi ya Koroshokurudishwa wizarani
Bodi ya Koroshokurudishwa wizarani
RAIS Dkt. John Magufuli ameitaka Wizara ya Kilimo ijitathmini kutokana na suala la mauzo ya zao la korosho linavyoendelea pamoja na utendaji wa Bodi ya Korosho Tanzania.
Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kumrudisha wizarani Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Prof. Wakuru Magigi baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Oktoba 26, 2018) katika kikao chake na wakuu wa mkoa ya inayolima korosho kilichofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.“Haturidhishwi na utendaji wa bodi ambao amekiuka maelekezo ya msingi ya Serikali katika kusimamia mfumo mzima wa zao la korosho uliopelekea kuvurugika kwa minada.”
Kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imesitisha minada yote ya korosho nchini kuanzia leo na kuwataka wakulima wawe watulivu wakati ikishughulikia suala hilo.Kiongozi huyo wa Bodi ya Korosho analalamikiwa kwa kufanya kazi bila ya kushirikisha ushirika wa zao hilo na kutotambua mamlaka zilizowekwa kisheria kama mkuu wa mkoa.
Mbali na malalamiko hayo pia anadaiwa kuendesha operesheni kwa kutumia silaha na askari dhidi ya viongozi wa ushirika kinyume cha taratibu za nchi.
Hivyo, Waziri Mkuu amemuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi na wa Mtwara wahakikishe gari lenye namba T 814 DDM pamoja na dereva wake linatafutwa popote.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba.
Washirki wa Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa uliowajumuisha Wakuu wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...