Na Mwandishi Wetu, Uvinza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kuwaondoa katika
madaraka Mkuu wa Utawala wa Jeshi l aPolisi Mkoa wa Kigoma
ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Operesheni
wa Mkoa huo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza na Mkuu wa Intelejinsia
wa wilaya hiyo.
Pia Lugola ameagiza askari wote wa kituo cha polisi Mpeta na Nguruka
wilayani vinza wwahamishwe haraka iwezekanavyo katika vituo hivyo.
Lugola ametoa kauli nzito kwa kuwaondoa katika nyadhifa zao maafisa
wa juu wa jeshi hilo, kutokana na mapungufu aliyoyaona katika
operesheni iliyofanyika mwezi uliopita ya kuwaondoa wakulima na
wafugaji waliovamia ranchi za Taasisi ya NARCO ambao ipo chini ya
Wizra ya Mifugo, ambayo katika operesheni hiyo askari polisi wawili na
raia wawili waliuawa.
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Kitongoji cha Mwanduhubandu, Kijiji cha Mpeta Wilayani Uvinza,
leo, Waziri Lugola alisema viongozi hao wa Polisi wameshindwa
kuifanya kazi hiyo kwa umakini ndio mana kulikua upungufu mkubwa
katika operesheni hiyo, hivyo damu za waliouawa zinakua juu ya hao
viongozi wa polisi mkoa na wilaya.
“Kutokana na hali hiyo, namuagiza IGP Sirro kuwaondoa kwenye
madaraka hao wote niliowataja ifikapo kesho, na kesho Jumatatu
nitakapo kuwa Dodoma nitakutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuona hatua nyingine za kinidhamu
zitakazochukulia kwa hao niliowataja,” alisema Lugola.
Waziri Lugola aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi halina nia ya kuua mtu,
kumuonea mtu, kudhulumu mtu lakini pale inapotokea jeshi hilo
limeshindwa kutekeleza wajibu wake vizuri, lazima yeye Waziri achukue
hatua.
Hata hivyo, Lugola alisema Jeshi la Polisi halipaswi kuvunjika moyo,
litaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika kuhakikisha
linapambana na uhalifu, kwa hayo ambayo yanayojitokeza hayana
nafasi ya kuwakatisha tamaa wala kuwavunja moyo.
“Mimi Waziri wa Wizara hii, dhamana yangu na haya ninayoyafanya,
vyombo vyangu vya ulinzi na usalama ninavyovisimamia msinione mimi
kama mwanasiasa, msichukulie maagizo yangu na matamko yangu
kama ya mwanasiasa, atyakaye jidanganya hivyo, itakula kwake,”
alisema Lugola.
Lugola alioagiza waondolewe madaraka ni Mkuu wa Utawala wa Jeshi l
aPolisi Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wakati operesheni hiyo ilipotokea, ACP Simon Ngowi, Mkuu wa
Operesheni wa Mkoa huo, SP Msembele, Mkuu wa Polisi Wilaya ya
Uvinza, SSP Mwakisambwe, na Mkuu wa Intelejinsia wa wilaya hiyo,
InspektaDotto Daudi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...