Katika kuendeleza mafanikio makubwa na ya kipekee kwa msimu wa 11  ya maonyesho  ya jukwaa la mitindo (SWAHILI FASHION WEEK) ambalo ni la kipekee Afrika mashariki, maandalizi yafunguliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Mbunifu  wa mitindo nchini Mustafa hassanali amezungumza na wadau, wabunifu pamoja na wanahabari kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa rasmi tarehe   30 mwezi huu mpaka tarehe 2 disemba katika  ukumbi wa makumbusho ya taifa posta na amesema kuwa maandalizi ya mwaka huu ni ya kusisimua na kufurahisha sababu kazi za mitindo zipo na ni za hali ya juu .

Hassanali  amesema kwa utiifu wote  lengo la kuendeleza na kuimarisha  nafasi ya mitindo kwa Afrika  linabaki kuwa mbele,kupitia jukwaa hili na mchango mkubwa wa waandishi wa habari tutaendelea kuunga mkono vipaji  vilivyopo katika sekta ya mitindo.


Aidha,amefafanua zaidi licha ya kuunga mkono kuendeleza vipaji bali pia kutengeneza na kukuza soko la kimataifa na ndio sababu kuu ya kuunga mkono kutekeleza juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Katika sera ya kuelekea uchumi wa viwanda kupitia bidhaa za nguo zilizotengenezwa Tanzania.

Alikadhalika balozi wa italia nchini Tanzania Robert Mengoni amesema ifike pahala kila mtu aheshimu kazi za Ubunifu wa mitindo kama biashara kutokana na wabunifu kuwekeza na kupata vipato vya kuendesha maisha yao pamoja na familia kupitia Ubunifu huo.      kwa upande wa mwakilishi wa baraza la Sanaa (BASATA) Vivian shalura amepongeza juhudi zinazofanywa na mbunifu huyo mahiri katika mitindo ambae amekua akifata sheria pamoja na vibali huku akiwa amejisajiri kikamilifu.

Shalua amewataka wabunifu chipukizi wajaribu kubuni nguo ambazo hazitawabugudhi au kudharirisha watazamaji,pia amewashauri wabunifu kukuza lugha yetu ya kiswahili kupitia baadhi ya Nguo ambazo majina yake yanatokana na kiswahili chetu kama vile mshono wa mwanamke nyonga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...