Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kikosi cha Yanga kimewasili Visiwani Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi lililoanza kutimua vumbi Januari Mosi 2019 na kufikiwa tamati Januari 13, 2019.
Kikosi hicho kinaongozwa na Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila akisaidiwa na Kocha wa timu ya Vijana Said Maulid 'SMG', daktari wa timu Edward Bavu, Meneja wa timu Nadir Haroub "Canavaro" na Mohamed Ali.
Yanga watashuka dimbani kesho saa 2.15 wakiumana na KVZ ukiwa ni mchezo wa kwanza kwenye mashindano hayo kwenye dimba la Amani Zanzibar. Wachezaji hao ni
1. Maka Edward
2. Haji Mwinyi
3. Said Makapu
4. Matheo Anthony
5. Erick Msagati
6. Deo Mkami
7. Ibrahim Abrahaman
8. Ibrahim Ahmed
9. Deus Kaseke
10. Mustapha Seleman
11. Abuu Shaban
12. Ramadhan Mrisho
13. Mohamed Salumu
14. Cheda Hussein
15. Yasini Salehe
16. Salumu Mkama
17. Faraji Kilaza
18. Bakari Athman
19. Said Khasimu
20. Shaban Mohamed
21. Jafari Mohamed
22. Pius Buswita
23. Juma Abdul
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...