Na
Benny Mwaipaja, WFM, Kibaha
Serikali imetoa zaidi ya
sh. bilioni 42 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Sekondari 42 kati
ya shule 88 kongwe zilizopo nchini kote ikiwemo shule ya Sekondari Ruvu iliyoko
Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa shule hiyo,
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la
Serikali ni kuhakikisha kuwa shule zote Kongwe ambazo zinahistoria kubwa ya
kutoa viongozi wengi na wataalam mbalimbali nchini, zinakuwa na hadhi na kuwa
kimbilio la wananchi.
Ametoa wito kwa uongozi wa
shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa
kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ili thamani ya uwekezaji mkubwa wa
Serikali unaofikia zaidi ya shilingi milioni 990 uweze kuonekana
"Dhamira yetu ni
kuona watoto wetu wanasoma kwenye mazingira sahihi na ufaulu wao unaongeeaka
kwa sababu tunawaandaa wataalam wa kesho wa Taifa letu" Aliosisitiza Dkt.
Kijaji
Alisema amejionea
ukarabati uliofanyika shuleni hapo ambapo pamoja na shilingi milioni 992
kutumika katika ukarabati huo, bado nyumba 6 za walimu hazijakarabatiwa pamoja
na kutonunuliwa kwa samani za shule vikiwemo vitanda na kuahidi kuifanyia kazi
changamoto hiyo wakati wa huu wa mchakato wa bajeti mpya
Kwa upande wao, Mbunge wa
Kibaha Vijijini, Hamoud Juma na Mkuu wa Shule hiyo, Juliana Chimazi, wameishukuru
Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha shule hiyo na kuomba wapatiwe
fedha kwa ajili ya kununulia samani hasa vitanda kwa ajili ya wanafunzi ili
kwenda sambamba na uboreshaji mkubwa wa majengo uliofanyika shuleni hapo.
Mkuu wa shule hiyo Mwl.
Juliana Chimazi alimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji
kwamba shule hiyo inahitaji vitanda vipya kwa kuwa vilivyopo vimedumu zaidi ya
miaka 50 pamoja na kuomba fedha kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa nyumba
sita za walimu.
Miongoni mwa miundombinu
iliyoboreshwa katika shule hiyo ya Sekondari ya washichana Ruvu ni pamoja na mifumo
ya maji taka, madarasa, vyoo, mabweni, nyumba za walimu na Ofisi.
Naibu Waziri Dkt. Kijaji
anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali iliyopewa fedha na
Serikali ikiwemo ya kimkakati inayolenga kuziwezesha Mamlaka za Serikali za
Mitaa nchini kujitekemea kwa mapato.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili
kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya
Wasichana Ruvu Mkoani Pwani, kuhakikisha maboresho ya shule hiyo
yanakwenda sambamba na ufanisi katika utoaji taaluma, wakati alipofanya
ziara ya kikazi ya kukagua uboreshaji huo. Kulia ni Mbunge wa Kibaha
Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana
Chimazi. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akikagua maboresho ya Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wa pili kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, watatu kushoto ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi.
Muonekano wa Bweni la wanafunzi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ambapo Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi, aliomba Serikali isaidie katika kuboresha miundombinu ya nyumba 6 za walimu ambayo haijakarabariwa baada ya fedha sh. milioni 990 kumalizika kabla ya kazi hiyo kukamilika.
Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, akitoa ufafanuzi wa namna walivyosimamia fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wakati wa ziara yua kikazi ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani Bw. Shaibu Mangalu, akielezea namna Shule hiyo ilivyotumia utaratibu wa shule hiyo kwa njia ya Force Account uliogharimu takribani Sh. milioni 992, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipotembelea na kukagua maboresho hayo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Viongozi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ,baada ya kukagua uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo .Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...