Na Shushu Joel, Mkuranga.
MBUNGE wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi amepokea msaada wa mifuko 120 ya saruji kutoka kwa shirikisho la walimu makada wa chama cha mapinduzi (CCM).
Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko hiyo mratibu wa shirikisho hilo Bakari Msingili alisema kuwa kusudi la wao kufanya uamuzi huo ni kutokana na juhudi za kimaendeleo zinazo fanywa na Mbunge huyo kwenye nyanja za elimu,Afya na miundombinu kwenye wilaya ya mkuranga.
Aliongeza kuwa imekuwa ngumu kuamini kwa kile ambacho tunakifanya kama walimu juu ya kuchangia fedha kwa ajili ya maendeleo kutokana na tabia iliyojengeka kwa watu kuwa walimu ni kundi la watumishi ambao ni wabaili sana.
"Mifuko hii ya saruji itasaidia kwenye nyanja hii ya elimu lakini hata sie kama shirikisho la walimu makada wa ccm" Alisema Bakari.
Naye Afisa elimu ya watu wazima Mektrida Kahindi ambaye ni mjumbe wa shirikisho hilo alisema kuwa shirikisho hilo litaendelea kutoa misaada mbalimbali katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia maendeleo kwenye wilaya ya mkuranga.
Aliongeza kuwa mifuko hii ya 120 ya saruji ni mwanzo tu lakini kuna mambo makubwa ya nakuja mbele yetu.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Ulega amewapongeza wana shirikisho hilo kwa kutambua juhudi wanazozifanya jimbo humo hivyo amewataka wananchi wake kutumia kwa uangalifu saruji hizo kwani mwezi wa kumi watakuja ili kuhakikisha usahihi wa kazi jinsiilovyoondoka
Aidha Ulega amewapongeza walimu hao kwa kuridhishwa na kuona kile kinachofanwa na Serikali ya awamu ya tano china ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Aidha Ulega amewataka walimu kuunda vikundi ili kupata mikopo ya wanyama kama ng'ombe na mbuzi ili waweze kuwaingizia kipato cha ziada mbali na kutegemea mshahara.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (wapili kuliua )akipokea mifuko 120 ya saruji kutoka kwa shirikisho la walimu makada wa chama cha mapinduzi (CCM)(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga kulia na Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (wapili kulia) wakiwapongeza walimu makada wa chama cha mapinduzi (CCM kwa kukabidhi mifuko 120 ya saruji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...