Wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha mikoa mingi kujitosheleza kwa mafuta ya kula.
Kauli
hiyo imetolewa leo Ijumaa mjini Kigoma na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw. Gerald Kusaya alipoongea na waandishi wa habari kuhusu ziara ya
Waziri Mkuu .
" Jitihada
za Wizara hadi sasa tumeweza kuzalisha mbegu bora za michikichi
1,556,111 ambapo miche 49,032 ipo tayari kwa ajili ya kupandwa kwenye
Halmashauri sita za Mkoa wa Kigoma" , alisema Kusaya.
Katibu
Mkuu huyo amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ( Mb) kesho Jumamosi
anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Kigoma kwa lengo
la kugawa miche bora ya michikichi kwa wakulima na vikundi vya AMCOS .
Aidha,Waziri
Mkuu Majaliwa atazindua rasmi zoezi la upandaji miche bora ya
michikichi katika Gereza la Kwitanga na kambi ya JKT Bulombora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...