Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akifurahia pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi
la Magereza muonekano wa majengo mapya ya Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi
cha Karanga alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Mkoani
Kilimanjaro. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea Kashimba.

Muonekano wa
jengo jipya la kiwanda cha bidhaa za Ngozi cha Karanga kilichopo katika
Gereza la Karanga Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akikagua miundombinu ya Kiwanda cha Bidhaa za
Ngozi cha Karanga alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Moshi, Mkoani
Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kutoka kulia) akiongozana
na Wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za Ngozi
kilichopo katika Gereza la Karanga lililopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujezi wa kiwanda hicho.

Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa
Kiwanda cha bidhaa za Ngozi cha Karanga alipotembelea Kiwanda hicho
kukagua maendeleo ya ujenzi.

Baadhi ya
Wasimamizi wa Mradi huo wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).

Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua baadhi ya mishine za
kuchakata bidhaa za Ngozi alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa kiwanda hicho.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU) OWM-KVAU
***************************
Na Mwandishi Wetu, Moshi.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametoa pongenzi kwa Jeshi la
Magereza na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa
hatua waliyofika katika ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za Ngozi cha
Karanga.
Akizungumza mara
baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo wa ujenzi wa kiwanda hicho
uliopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro ambapo hatua za ujenzi umefikia
asilimia 97 Waziri Mhagama alieleza kuwa mikakati ya Serikali ya Awamu
ya Tano inayoongozwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ni kuendeleza uchumi wa Taifa kupitia Viwanda.
“Mradi huu wa
ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha bidhaa za Ngozi hapa Karanga ni mmoja ya
utekelezaji wa miradi ya kimkakati ambayo inatekelezwa na Serikali ya
Awamu ya Tano na utakuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine utakapoanza
uzalishaji wa bidhaa za Ngozi ambazo zitakuwa zinazalishwa hapa nchini,”
alieleza Mhagama.
“Nimeridhika na
kasi ya ujenzi wa mradi huu, na nitoe pongezi zangu kwa Jeshi la
Magereza linalosimamia ujenzi wa mradi huu kwa kushirikiana na Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii (PSSSF) hatua mliyofikia kwa kweli ni nzuri,”
Alisema
Mhagama Alifafanua kuwa,
Kiwanda hicho kitakavyo kamilika mapema kitakuwa na manufaa makubwa kwa
taifa ikiwemo kutoa fursa za ajira kwa Watanzania pamoja na kuongeza
mapato ya Serikali kupitia bidhaa zitakazokuwa zinazalishwa na kiwanda
hicho kuuzwa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa
kukamilika kwa majengo manne ya msingi katika kiwanda hicho ina ashiria
kuwa hatua iliyobaki sasa ni kusimikwa mitambo ya uchakataji wa ngozi
ili kiwanda hicho kiweze kuanza kazi ya uzalishaji haraka.
Aidha, Waziri
Mhagama ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma kuhakikisha anasimamia kwa karibu matumizi ya fedha ya
mradi huo.
“Ujenzi wa mradi
huu umefikia asilimia 97 na matumizi ya fedha yanaridhisha ikionesha
kwenye kumbukumbu zenu kuwa kuwa hadi sasa asilimia 63 ya malipo
yamekishafanyika, hivyo suala la ‘Value for Money’ limeweza kutekelezwa
katika mradi huu,” alisema Mhagama.
Pia Mheshimiwa
Mhagama alielezea namna alivyofurahishwa na utekelezaji wa mafunzo ya
vitendo sehemu za kazi ambayo yamekuwa ni chachu ya kuwawezesha vijana
kukuza ujuzi walionao.
“Katika mradi wa
ujenzi wa kiwanda hiki nimefurahi kuona vijana ambao wanataaluma ya
uhandisi wameweza kushiriki na kutoa mchango wao katika mradi huu wa
muhimu kwa taifa ambao umewawezesha kupata ujuzi na wameonyesha namna
walivyojitoa katika kujenga nchi yao,” alisema Mhagama.
Kwa Upande
wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, RPO Dkt. Miraji
Katumbily alieleza kuwa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 97 na
hatua iliyobaki sasa ni pamoja na kusimikwa kwa mashine ya uchakataji,
kuweka miundombinu ya umeme, vifaa vya TEHAMA na kukamilisha ofisi ili
uzalishaji katika kiwanda hicho uanze rasmi.
Naye Mkurugenzi
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Hosea
Kashimba alimuhakikishia Waziri huyo kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na
Jeshi la Magereza nchini kuwa watatekeleza maagizo yote yaliyotolewa
ili kuhakikisha mradi huo unakamilika bila kuwa na kasoro zozote.
Wakati huo huo,
Kijana mmoja wapo anayejitolea kwa mafunzo ya vitendo katika mradi huo
Mhandisi Edward Chalamila alimshukuru Waziri kwa Ofisi yake kuweza
kutambua umuhimu wa Programu hiyo ambayo imekuwa na manufaa kwa vijana
katika kukuza ujuzi wa fani walizozisomea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...