Edouard Mendy.

Na Lusajo Frank, Michuzi Tv
KLABU ya Chelsea ipo katika mazungumzo na uongozi wa klabu ya  Rennes ya nchini ufaransa kuinasa saini ya mlinda mlango wa klabu hiyo Edouard Mendy mweny umri wa mika 28 kwa dau la Paundi Milioni 18.

Ikiwa ni harakati za  kuongeza chachu ya ushindani katika
Miamba hiyo ya jiji la London.

Inasemekana  kuwa  inatarajiwa kumshawishi mlinda mlango huyo kupitia Mkurugenzi wa ufundi Peter Cech ambae ana uhusiano wa karibu na klabu hiyo ya Ufaransa.

Chelsea ilimaliza nafasi ya nne msimu uliopita 2019/20 na kuruhusu idadi ya magoli 54.

Hivyo Ujio wa Edouard Mendy huenda ukasaidia kupunguza idadi ya magoli kwa msimu mpya wa 2020/2021 unaotarajiwa kuanza September 12.

Kocha wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard (Super Frank) amepania  kufanya marekebisho makubwa ndani ya kikosi chake kwa kusajili wachezaji wapya, Hakim Ziyech, Tim Werner, Kai Havertz nk.

Ikumbukwe The blues walimaliza msimu uliopita 2019/2020 pasipo kombe lolote, hivyo ujio wa wachezaji wapya utaongeza chachu ya ushindani ndani ya kikosi na kushinda mataji msimu ujao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...