Uongozi wa klabu ya KMC FC umetoa mapumziko mafupi kwa wachezaji wake kuanzia Mei 17 na kwamba watapaswa kurejea kambini Mei 25 ili kuendelea na maandalizi ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Dododma Jiji.

Mapumziko hayo yametokana na Timu ya KMC FC kutokuwa na mchezo wowote wa mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja ambapo kwa mujibu wa ratiba ya Bondi ya Ligi ni kwamba KMC FC itaendelea na mchezo wa Ligi Kuu kuanzia Juni 17 mwaka huu katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma dhidi ya Dodoma Jiji.

Aidha kufuatia mapumziko hayo, Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo wataweka utaratibu wa kufanya mazoezi pindi wachezaji watakaporejea kambini sambamba na kucheza mechi nyingi za kirafiki kwa lengo la kuendelea kujiimarisha na hivyo kufanya vizuri kwenye michezo iliyobakia.

“Tumetoka kupoteza mchezo muhimu dhidi ya Azam FC , lakini bado haitukatishi tamaa kuendelea kupambania nafasi ya Nne, hivyo mapumziko haya ni maalumu kwa wachezaji wetu, na kwamba tukirudi kama Timu uongozi kwa ujumla tutaendelea kuweka nguvu zaidi kwenye michezo yetu iliyobaki na hivyo kufanya vizuri ili mwisho wa siku tufikie malengo ambayo tumejiwekea.

Hata hivyo KMC FC hadi sasa imecheza michezo 29 na kufikisha alama 41 na kuendelea kusalia katika nafasi ya tano huku ikiwa imebakiza michezo mitano kabla ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu soka Tanzania bara 2020/2021, ambayo ni dhidi ya Dodoma Jiji, Mtibwa Sugar, JKT Tanzana , Simba pamoja na Ihefu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...