EQUITY Bank imesema kuwa inajivunia kuwa Wadhamini Wakuu wa Full moon party iliyofanyika katika hoteli ya Kendwa Rocks, Zanzibar.
Udhamini huo ulikuwa na nia ya kuleta suluhisho la kufanya malipo kwa wepesi kupitia kadi yake ya malipo "Eazzy Card" ambayo ni kadi ya malipo ya awali iliyongishwa na mtandao wa malipo wa VISA.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Equity Bank inaeleza kuwa Eazzy Card ni rafiki wa malipo hasa kwa kipindi hiki cha Covid-19 kwa sababu ina huduma ya "Tap and Go" hivyo kupunguza migusano na foleni zinayotokea wakati wa kufanya malipo.
Eazzy Card kutoka Equity Bank ni kadi kwa ajili ya mtanzania yoyote na huhitaji kuwa na akaunti ya Equity ili kuipata. Eazzy card inatumika popote duniani kwenye mfumo wa VISA. Tembelea matawi au Wakala wa Equity Bank aliye karibu ili kujipatia kadi yako ya Eazzy Card.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...