Na Mwandishi Wetu Namtumbo

 

Wananchi wa Kata ya Mkongo Kata ya Mkongo Wilayani Namtumbo wameiomba Wizara Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kukarabati na kuwapatia wahudumu katika kituo cha Afya Mkongo ambacho kinahudumia Kata Sita.

 

Hayo yamebainikia wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

 

Akizungumza mara baada ya kusikiliza kero hiyo Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amewaahidi wananchi hao kulitatua tatizo hilo la ukaratabi wa majengo na upungufu wa wahudumu wa Afya.

 

"Nimeona hali halisi katika kituo hiki cha afya umbali kufika hapa huduma hii ni muhimu sana hili tutalifanyia kazi "alisema Mhe. Mwanaidi 

 

Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amewahakikishia Wazee kupata huduma za Afya kwa kipaumbele katika vituo vya Afya kwani ni kundi maalum linaloaangaliwa na Serikali kwa ukaribu.

 

Kituo hicho cha Afya kina zaidi ya miaka thelathini hakijafanyiwa uakarabati mkubwa na kiahudumia wananchi wengi zaidi ya uwezo wake.

 

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na wananchi wa Kata ya Mkongo alipotembelea Kituo cha Afya katika Kata hiyo Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...