Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi, David A. Misime - SACP akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma na kuonesha jezi feki.

JESHI Jeshi la Polisi limekamata jezi feki  zinazouzwa zinazotumiwa na timu mbalimbali za hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi, David A. Misime - SACP amesema utengenezaji na uuzaji wa jezi feki (zisizo na kiwango) ni kosa la jinai na kibaya zaidi wanaofanya hivyo wanakuwa ukwepaji kulipa kodi kwa sababu hazipitii katika mfumo ulio rasmi.

Misime - SACP amesema baadhi ya timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huingia mikataba na kampuni mbalimbali ya kutengeneza jezi na pale zinapouzwa kiasi fulani huingia katika timu ili kugharamia mahitaji ya wachezaji kama mishahara.


Amesema Timu ya Polisi Tanzania imefanya hivyo kwa kuingia mkataba na baadhi ya kampuni kama vile Lodhia Group of Companies na Kampuni ya Vunja Bei.

Kwa bahati mbaya na kwa nia ovu ya kujipatia fedha kinyume cha sheria za nchi, baada ya timu hizo kuingia mikataba, utengenezaji, usambazaji na mauzo yanapo anza wapo watu wanaotengeneza jezi zilizo chini ya kiwango (jezi feki) kwa kutumia nembo zilezile na kuanza kuziuza mitaani. Kwa kufanya hivyo huinyima serikali mapato na kibaya zaidi timu hukosa fedha zikiwepo za kuwalipa wachezaji.

amesema  msako ulioendeshwa na Jeshi la Polisi watuhumiwa 15 wameshakamatwa kutoka maeneo ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Tabora na Tunduma ambapo jumla ya Jezi feki 279, Urembo (ribons) 300 na Kofia 6 zimekamatwa. Kesi zimefunguliwa dhidi yao na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha katika uchunguzi uliofanyika imebainika kuwepo na wafanyabiashara waliofanya mawasiliano na viwanda vya ndani na nje ambavyo jezi halali hutengenezwa wakitoa oda ya kutengenezewa jezi feki. Hawa nao ambao jumla yao ni 11 wamefunguliwa jalada, wamehojiwa na ushahidi unaendelea kukusanywa.

Amesema Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa watu wanaofanya hivyo kuacha mara moja kwani watachukuliwa hatua endapo wataendelea kufanya uhalifu huo.

Aidha ametoa wito kwa timu ambazo zitabaini watu wanaotengeneza na kuuza jezi feki zenye nembo walizokubaliana katika mikataba walioingia na kampuni wasisite kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watu hao.

Pia amewaasa Watanzania, wanapo nunua jezi za timu wanazozipenda na kuzishabikia, wanunue kwenye maduka stahiki na pale watakapo baini kuuziwa jezi feki wasisite kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi. Wananchi tunaomba watambue jezi hizo feki wanauziwa bei ile ile ya jezi halali, ambazo ukitumia hazidumu kama zile halali.

Tukumbuke tatizo la bidhaa bandia (feki) ni la dunia nzima, tukilifumbia macho hili la jezi feki wahalifu wana tabia ya kunogewa, watahamia hata katika dawa za kutibu binadamu, mifugo na hata katika vifaa mbalimbali vya matumizi ya binadamu na madhara yatakuwa kwetu sote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...