Na Abdullatif Yunus - Michuzi Kagera.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso (Mb) amekiri kuwepo kwa upungufu wa maji safi na salama Wilayani Ngara mara baada ya Kuwasili Wilayani humo Februari 24, 2022 Siku moja baada Rais Samia kumtaka Waziri Aweso kufika na kubaini changamoto za Maji.

mara baada ya kuwasili Wilayani Ngara Waziri Aweso amebaini Upungufu wa Maji safi na salama unaosababishwa na kutokamilika kwa baadhi ya miradi inayoendelea kutekelezwa changamoto kubwa ikiwa ni kasi ya kukamilisha miradi.

Akizungumza na Watumishi Viongozi na Wadau wa Maji katika Ukumbi wa Halmashauri ya Ngara amekaririwa akisema, "..hapa Ngara mnayo maji lakini siyo toshelezi, mahitaji ya Maji ni lita Milioni 2.8 uwezo wa  mitambo yetu kuzalisha Maji ni  lita 1.5 kwahiyo kuna upungufu wa lita Milioni 1.3 kwahiyo maji yapo lakini si toshelevu, Mhe. Mbunge baada ya kuingia aliliona hili kama mwakilishi, na ni mfuatiliaji.

Aweso amesema kupitia Juhudi za Mbunge Ndaisaba ambaye amekuwa akifuatilia mara kwa mara kuhakikisha azma ya  Wanajimbo wake wanapata maji, tayari Serikali imetenga zaidi ya Bilioni Nne kuhakikisha huduma ya maji inaimarika na kwamba kwa mradi alioekekeza Mhe. Rais Samia ukamilike kwa haraka utakamilika na kazi itafanyika usiku na mchana.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...