NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewataka Maafisa Waandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kufanya jitihada kubwa za kuzuia mianya ya rushwa kabla haijatokea.

Ndejembi ametoa kauli hiyo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wakati akifunga mafunzo ya Maafisa hayo hayo yaliyokua yanatolewa kwa ajili ya kuwajengea uelewa na utimamu kazini ambapo amewataka kuwa waadilifu na wazalendo kwa Nchi yao.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Naibu Waziri Ndejembi amesema ni vema maafisa hao kuhakikisha wanazuia mianya hiyo kabla haijatokea na siyo kuanza kupambana baada ya kutokea kwa kuhakikisha wanasimamia vema miradi ya serikali ikiwa ni pamoja na kukagua thamani ya fedha kwenye miradi inayotekelezwa na Serikali.

" TAKUKURU mnafanya kazi nzuri lakini niwatake kutumia mafunzo haya ya Uongozi mliyoyapata kwenda kuhakikisha mnatekeleza maelekezo ya Rais Samia lakini vilevile mnafuata Sheria, Taratibu na Kanuni katika kufanya majukumu yenu. Na zaidi endeleeni kutoa elimu kwa wananchi ili tuwajengee watu wetu uelewa mpana wa kuona rushwa ni kitendo kisicho cha kizalendo na waichukie.

" Kupitia mafunzo haya mnapaswa sasa kuacha kufikiria kupambana na rushwa tu bali muangalie namna gani ya kuzuia isitokee, kagueni miradi ya serikali inayotekelezwa kwenye Halmashauri na Mikoa yenu, tazameni thamani ya fedha iliyotumika, zuieni ubadhirifu ili fedha ya Serikali ifanye yale yaliyokusudiwa kwa wananchi na siyo kufaidisha wachache.

Nyinyi TAKUKURU hampaswi kusubiri mpaka viongozi wakuu waje watembelee miradi ndio waone kuna ubadhirifu watoe maelekezo kwenu, Rais Samia anatekeleza miradi mikubwa kila kona ya Nchi yetu ni jukumu lenu kumuunga mkono kwa kuisimamia ili asiwepo mtu ambaye atajinufaisha tumbo lake," Amesema Ndejembi.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...