Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa mradi wa maboresho ya elimu juu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk.Francis Michael akizungumza kuhusiana na mradi wa maboresho ya elimu ya Juu (HEET) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizindua mradi wa HEET jijini Dar es Salaam.



Picha mbalimbali za wakuu wa vyuo na wahadhiri katika uzinduzi wa mradi wa HEET Jijini Dar es Salaam.

*Benki ya Dunia yaahidi kuendelea ushirikiano Tanzania

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa katika maboresho ya elimu ya juu kwa vyuo vikuu kwenda katika masuala ya kukwamua vijana kiuchumi kwa kutoa elimu wezeshi wa vijana hao kufikia katika uchumi wa uzalishaji.

Katika kufika malengo hayo serikali imekuja na maboresho hayo kwa kutoa ufadhili wa kuwasomesha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu nje ya nchi Ili kusaidia kutoa elimu ujuzi yenye kiwango bora kuendana na soko la ajira kimataifa pamoja na uwezo huo utumike katika kuwafundisha wanafunzi wa elimu ya juu.

Hayo ameyasema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa HEET wa miaka mitano uliolenga kuboresha elimu na kunufaisha vyuo 14 ambapo amesema kupitia mradi huo pia unakwenda kusaidia Wahadhiri kwenda kusoma katika nchi mbalimbali ikiwemo Denmark,Ufaransa,Ubelgiji, Ili kusaidia kuongeza ubora wa Elimu na lazima ianzie juu ndipo ishuke sekondari hadi shule za msingi kwani dunia Sasa hivi imebadikika kinachohitajika ni ujuzi zaidi.

"Duniani kote wanazungumzia suala la elimu hii inatokana na changamoto ya kuwa na wahitimu wengi lakini wanaoshindwa kujiajiri kutokana na kutokuwa na ujuzi ukitazama vyeti wanavyo lakini digree za kutosha lakini mwanafunzi inashindikana kuajiajiri hivyo Wahadhiri waliopata fursa kwenda kusoma njeem wakihitimu wanaokuja kubadilisha mtazamo mtazamo wa wanafunzi kuingia katika elimu ujuzi" amesema Waziri Mkenda

Profesa Mkenda amesema Mradi huo ni mkubwa na ni umekuja kutoa hamasa na kusukuma Tanzania katika suala zima la elimu ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya vyuo pamoja na mitaala.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael amewataka wasimamizi wa mradi kuhakikisha fedha zikizotolewa za mradi zinatumika katika mlengo uliokusudiwa kwani ikibainika kuna kuwa watu wanafanya vinginevyo watakaohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria kwani huko kunakuwa kurudisha malengo ya serikali.

Amebainisha kuwa fedha zikizotolewa jumla ya dola Milioni 425 sawa na Bilioni 972 zilizotolewa na Benki ya dunia ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu Kwa lengo la kuboresha elimu ya juu nchini.

"Vyuo vikuu havijafikia kiwango kilichowekwa kwa wahitimu wa elimu ya juu kwani mpaka sasa ni asilimia 3.5 ambapo lengo ni kufikia asilimia 12 huku akitaka kamati ya wasimamizi wa mradi huu kutosita kutoa taarifa ya changamoto yeyote itakayowakabili ili kwenda kwa kasi kwenye utekelezaji "amesema Dk.Michael

Naye Mwakilishi kutoka benki ya Dunia Preeti Arora ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na mtazamo chanya wa kuboresha elimu Ili kuendana na mahitaji ya Soko la ajira la kimataifa hivyo watahakikisha wanashirikiana nao bega kwa bega pale watakapohitajika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...