Na Said Mwishehe, Michuzi TV
UBALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania kupitia Mfuko wa mshikamano wa Serikali ya Ufaransa kwa miradi ya ubunifu (FSPI) umezindua mradi wa SANAAPRO kwa lengo la kusaidia tasnia ya ubunifu nchini ambapo kiasi cha Sh.bilioni 1.2 zitatumika kwenye mradi huo.
Akizunguza leo Septemba 28,2022, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kuwa mdhumuni ya jumla ya mradi huo ni kuendelea kusaidia tasnia ya ubunifu nchini Tanzania huku akieleza sekta hiyo imekuwa na mikakati ya kuvutia ili kuongeza ushindani, tija , ajira na ukuaji endelevu wa uchumi.
“Hakika ni uhai wa uchumi wa ubunifu zaidi ya hayo inatumiwa mara nyingi zaidi kukuza utangamano wa kijamii, maadili ya kijamii, ukuzaji wa kitamadubi na kama chanzo cha habari na maarifa,”amesema na kuongeza mradi huo ni kipaumbele cha Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.
“Hiyo inatokana na kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu sekta ya tasnia ya ubunifu , lakini pia katika mabadilishano ya wazi yaliyofanywa kati ya vijana wanaoshiriki sanaa na Rais Macron kwenye mkutano wa New Africa France uliofanyika Montpeller Oktoba mwaka 2021,”amesema.
Amefafanua kwenye tukio hilo la kihistoria Tanzania iliwakilishwa vyema na watu wa makundi mbalimbali wakiwemo ,wajasiriamali ,watetezi wa haki za binadamu, viongozi kutoka mashirika ya kiraia pamoja na mabingwa wa michezo. Ameongeza katika kipindi cha miaka miwili ijayo 2022/2023 mradi wa SANAAPRO utatekeleza shughuli mbalimbali ambapo walengwa wakiwa ni mashirika nane ya kitamaduni yanayofanya kazi kwa kushirikiano na mashirika matano ya Ufaransa.
Kwa upande wa Tanzania wanufaika ni ASEDEVA(Sanaa ya Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi Barani Afrika, MUDAFRICA ,CAC(Cultural Arts Centre)Arusha , Tuna-Present Tanzania, AJABU AJABU, DCMA-Zanzibar, Alliance Francaise Dar es Salaam, Foundation for Civil Society(FCS).
Aidha kwa nchi ya Ufaransa waliochaguliwa ni Wacheza dansi, Moise Toure/Francis Viet, IOMMA(Soko la Muziki la Bahari ya Hindi)La reunion ,Tamasha la Offcourts Trouville-Normandie, We Present-Marseille, Africolor-Paris.
Akielezea zaidi kuhusu lengo la SANAAPRO ni kufikia hatua muhimu ambazo ni program 15 za ruzuku ya moja kwa moja mnamo 2022/2023 , msururu wa mijadala 9 inayohusu sekta ya ubunifu , uwekezaji wa vifaa vya pamoja kwa mashirika manne ya kitamaduni, matukio ya ngoma, mafunzo ya wasanii 72 wa Hip hop kutoka Tanzania nzima, uzalishaji wa filamu fupi mbili za kiwango bora cha kimataifa.
"Mradi wa FSPI ni wa kibunifu katika nyanja kadhaa ikiwemo katika sekta ya ubunifu nchini Tanzania haijawahi kutokea awali, ni FSPI inayoshughulikia ukosefu wa usawa wa kijinsia katika mazingira ya tasnia na usimamizi kwa wanawake zimeundwa kwa hafla hiyo.
"Mradi hui unapendekeza kuangazia tasnia za ubunifu kama waundaji wa kazi barani Afrika na kama sababu ya utangamano wa kijamii.FSPI hii pia inafanya kazi kwa kusaidia uundaji na usambazaji wa kisanii kote nchini Tanzania ili kuchangia uwiano wa kijamii."
Aidha kushawishi mamlaka za Tanzania kuunda mfumo wa kisheria wa kulinda hadhi ya wasanii wa watanzania , kusaidia kuibuka kwa kizazi kipya cha watalaam wa kitamaduni na kuhimiza uwezeshaji wao.
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo kutoka MUDAFRICA, Rachel Kessi, alisema mradi huo utawasaidia vijana wa kitanzania wenye ndoto za kufikia mafanikio kwa ubunifu wanaoufikiria."Mradi huu umekuja katika kipindi sahihi kwa vijana, ubunifu wao utawapa mafanikio kwa fedha hizi ambazo Ubalozi wa Ufaransa wametoa," alisema Rachel.
Aidha, Mkurugenzi wa ASEDEVA,Isack Abeneko, alisema mradi huo pia utawahusisha wanawake na watu wenye ulemavu ambao nao watanufaika na mradi huo.
"Tunawashukuru sana wenzetu wa Ufaransa na nafasi hii , ASEDEVA hii ni nfasi kubwa ya kuwafanya vijana kufikia malengo yao hasa wale wenye ubunifu," alisema Abeneko.Mradi huo ulizinduliwa jana na balozi Hajlaoui utadumu kwa kipindi cha miaka miwili na kumalizka mwaka 2023.Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Nabil Hajlaoui (kushoto), akizungumzana waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mradi wa SANAAPRO,utakaosadia tasnia ya ubunifu hapa nchini, katika hafla iliyofanyikanyumbani kwake jijini Dar es Salaa jana kutoka kulia ni MkurugenziMtendaji wa Kampuni ya Asedeva, Isack Abeneko, Mkurugenzi wa Kampuni ya FCS, Arthur Mtafya, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mudafrika,Rachel Kessi
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
UBALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania kupitia Mfuko wa mshikamano wa Serikali ya Ufaransa kwa miradi ya ubunifu (FSPI) umezindua mradi wa SANAAPRO kwa lengo la kusaidia tasnia ya ubunifu nchini ambapo kiasi cha Sh.bilioni 1.2 zitatumika kwenye mradi huo.
Akizunguza leo Septemba 28,2022, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kuwa mdhumuni ya jumla ya mradi huo ni kuendelea kusaidia tasnia ya ubunifu nchini Tanzania huku akieleza sekta hiyo imekuwa na mikakati ya kuvutia ili kuongeza ushindani, tija , ajira na ukuaji endelevu wa uchumi.
“Hakika ni uhai wa uchumi wa ubunifu zaidi ya hayo inatumiwa mara nyingi zaidi kukuza utangamano wa kijamii, maadili ya kijamii, ukuzaji wa kitamadubi na kama chanzo cha habari na maarifa,”amesema na kuongeza mradi huo ni kipaumbele cha Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania.
“Hiyo inatokana na kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu sekta ya tasnia ya ubunifu , lakini pia katika mabadilishano ya wazi yaliyofanywa kati ya vijana wanaoshiriki sanaa na Rais Macron kwenye mkutano wa New Africa France uliofanyika Montpeller Oktoba mwaka 2021,”amesema.
Amefafanua kwenye tukio hilo la kihistoria Tanzania iliwakilishwa vyema na watu wa makundi mbalimbali wakiwemo ,wajasiriamali ,watetezi wa haki za binadamu, viongozi kutoka mashirika ya kiraia pamoja na mabingwa wa michezo.
Ameongeza katika kipindi cha miaka miwili ijayo 2022/2023 mradi wa SANAAPRO utatekeleza shughuli mbalimbali ambapo walengwa wakiwa ni mashirika nane ya kitamaduni yanayofanya kazi kwa kushirikiano na mashirika matano ya Ufaransa.
Kwa upande wa Tanzania wanufaika ni ASEDEVA(Sanaa ya Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi Barani Afrika, MUDAFRICA ,CAC(Cultural Arts Centre)Arusha , Tuna-Present Tanzania, AJABU AJABU, DCMA-Zanzibar, Alliance Francaise Dar es Salaam, Foundation for Civil Society(FCS).
Aidha kwa nchi ya Ufaransa waliochaguliwa ni Wacheza dansi, Moise Toure/Francis Viet, IOMMA(Soko la Muziki la Bahari ya Hindi)La reunion ,Tamasha la Offcourts Trouville-Normandie, We Present-Marseille, Africolor-Paris.
Akielezea zaidi kuhusu lengo la SANAAPRO ni kufikia hatua muhimu ambazo ni program 15 za ruzuku ya moja kwa moja mnamo 2022/2023 , msururu wa mijadala 9 inayohusu sekta ya ubunifu , uwekezaji wa vifaa vya pamoja kwa mashirika manne ya kitamaduni, matukio ya ngoma, mafunzo ya wasanii 72 wa Hip hop kutoka Tanzania nzima, uzalishaji wa filamu fupi mbili za kiwango bora cha kimataifa.
"Mradi wa FSPI ni wa kibunifu katika nyanja kadhaa ikiwemo katika sekta ya ubunifu nchini Tanzania haijawahi kutokea awali, ni FSPI inayoshughulikia ukosefu wa usawa wa kijinsia katika mazingira ya tasnia na usimamizi kwa wanawake zimeundwa kwa hafla hiyo.
"Mradi hui unapendekeza kuangazia tasnia za ubunifu kama waundaji wa kazi barani Afrika na kama sababu ya utangamano wa kijamii.FSPI hii pia inafanya kazi kwa kusaidia uundaji na usambazaji wa kisanii kote nchini Tanzania ili kuchangia uwiano wa kijamii."
Aidha kushawishi mamlaka za Tanzania kuunda mfumo wa kisheria wa kulinda hadhi ya wasanii wa watanzania , kusaidia kuibuka kwa kizazi kipya cha watalaam wa kitamaduni na kuhimiza uwezeshaji wao.
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo kutoka MUDAFRICA, Rachel Kessi, alisema mradi huo utawasaidia vijana wa kitanzania wenye ndoto za kufikia mafanikio kwa ubunifu wanaoufikiria.
"Mradi huu umekuja katika kipindi sahihi kwa vijana, ubunifu wao utawapa mafanikio kwa fedha hizi ambazo Ubalozi wa Ufaransa wametoa," alisema Rachel.
Aidha, Mkurugenzi wa ASEDEVA,Isack Abeneko, alisema mradi huo pia utawahusisha wanawake na watu wenye ulemavu ambao nao watanufaika na mradi huo.
"Tunawashukuru sana wenzetu wa Ufaransa na nafasi hii , ASEDEVA hii ni nfasi kubwa ya kuwafanya vijana kufikia malengo yao hasa wale wenye ubunifu," alisema Abeneko.
Mradi huo ulizinduliwa jana na balozi Hajlaoui utadumu kwa kipindi cha miaka miwili na kumalizka mwaka 2023.
Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Nabil Hajlaoui (kushoto), akizungumzana waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mradi wa SANAAPRO,utakaosadia tasnia ya ubunifu hapa nchini, katika hafla iliyofanyikanyumbani kwake jijini Dar es Salaa jana kutoka kulia ni MkurugenziMtendaji wa Kampuni ya Asedeva, Isack Abeneko, Mkurugenzi wa Kampuni ya FCS, Arthur Mtafya, na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mudafrika,Rachel Kessi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...