Na Mwandishi Wetu
SIMIYU Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko(CPB) , imefungua milango ya kufungua mazao kwa wakulima ikiwemo kuwafuata kokote walipo.
Hayo yalisemwa na Ofisa Masoko wa CPB, Frank Buberwa, kwenye maonyesho ya wiki ya chakula yanayofanyika mkoani Simiyu.
Buberwa alisema wamekuja na utaratibu huo kama moja ya njia ya kupunguza upatikanaji wa masoko ya mazao hayo ambapo imekuwa kilio cha muda mrefu cha wakulima pindi wanapofikia hatua ya kuvuna.
Mazao hayo ni pamoja na mpunga,maharage, ,jamii yote ya kunde na viungo mbalimbali.
Kuhusu kuyafuata mazao kokote yalipo,Buberwa alisema ni kutokana na wakulima wengine kukabiliwa na changamoto ya kutokuwa na fedha za kusafirisha au miundombinu mibovu walipo hivyo wameamua kumrahisishia kwa kuyafuata.
“Tunataka mkulima sasa ifike mahali afurahie kulima akiwa na uhakika wa kuuza mazao yake na niwahakikishie kuwa tuna uwezo wakununua tani zozote tutakazomkuta nazo mkulima,”alisema Buberwa.
Akilelezea viogezo vya kuuza mazao hayo,Ofisa Masoko na Usambazaji kutoka bodi hiyo, Fransisco Amos, alisema mazao hayo kutokuwa na unyevunyevu, mawe na yawe masafi.
Wakati kuhusu vipimo alisema watazingitia pande zote mbili kufaidika kwakufuata vipimo ambavyo vinatambulika na serikali.
Maonyesho hayo ya chakula yanayofanyika viwanja vya Halmashauri ya Simiyu, yameanza Oktoba 10 mwaka hyy na yanatarajia kufika kilele Oktoba 16 huku kaulimbiu yake ikiwa ni ‘Uzalishaji bora,lishe bora na maisha bora kwa wote,habaki mtu nyuma."
Muonekano wa Banda la CPB Simiyu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...