Na.Abel Paul- Jeshi la Polisi

Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMONI MWANGAMILO amewataka maderva wa vyombo vya moto kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo Pamoja nakufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara katika Mkoa wa Arusha.

Hayo amesemwa leo November 08 2022 wakati wa kukabidhi pikipiki kwa viongozi wa dini kutoka Manyara,Kilimanjaro Pamoja na Arusha ambapo amesema kuwa viongozi wanaowajibu wa kutibu mionyo ya wanadamu kiroho na kuwaomba kutokubali kuvuta na shetani wakati wa matumizi ya vyombo hivyo alisema Mwangamilo.

SP Solomon ameongeza kuwa wao kama Jeshi la Polisi wanawajibu kutoa Elimu kwa makundi yote ili kuwa na uelewa wa Pamoja na kukomesha ajali mkoa wa wa Arusha.

Kwa upandae wa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk BARNABAS MTOKAMBALI amesema lengo la kutoa vyombo hivyo ni kuwafikia waamini wa zehebu hilo na kutoa huduma ya kiroho na kazi za kanisa ikiwa ni Pamoja nakuongeza kasi ya maendeleo ya kanisa hilo

Wakati huo huo Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha SP SOLOMON MWANGAMILO amewata madereva wa vyombo vya moto maarufu mando wanaofanya safari zao nje ya jiji la Arusha na Kwenda maeneo ya vijijini kufanya marekebisho ya vyombo hivyo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.

Ametoa kauli leo Novemba 08.11.2022 kata ya Meserani wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha alipokuwa anazungumza na maderva wa vyombo hivyo ambapo amewataka kufanya marekebisho na kufuata sheria za usaklama barabarani ili kuondoa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo zinazosabishwa na vyombo hivyo maarufu Mando.










 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...