Waziri wa Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa mahafali ya 19 ya shule ya Msingi Betheli Mission iliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam leo Septemba 3, 2023.

Mkurugenzi wa Shule ya Betheli, Emmanuel Mshana akifafanua jambo kwa waziri wa Mipango na uwekezaji, Kitila Mkumbo leo katika Mahafali ya 19 ya Shule ya Msingi Betheli Mission iliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kanisa la Sabato Tanzania, Mchungaji Jurdon Mogela akifafanua jambo kwa waziri wa Mipango na uwekezaji, Kitila Mkumbo leo katika Mahafali ya 19 ya Shule ya Msingi Betheli Mission iliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa darasa la awali wakiwa katika Mahafali ya 19 ya shule ya  Msingi Betheli Mission iliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam leo Septemba 3, 2023.
Mmoja ya wanafunzi akitoa mahubiri kutoka katika Biblia leo Septemba 3, 2023  katika Mahafali ya 19 ya shule ya  Msingi Betheli Mission iliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam leo Septemba 3, 2023.
Baadhi ya wahitimu wakiingia katika eneo la Mahafali ya kuhitimu shule ya msingi  ikiwa ni Mahafali ya 19 ya shule ya Msingi Betheli Mission iliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam leo Septemba 3, 2023.
Baadhi ya Wazazi na walenzi wakiwa kwenye Mahafali ya 19 ya Msingi Betheli Mission iliyopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam leo Septemba 3, 2023.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI imesema inaunga mkono na itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi mbalimbali zikiwemo za dini kuwekeza katika elimu hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo Septemba 3, 2023 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo wakati wa Mahafali ya 19 ya Darasa la Saba ya shule ya Msingi na Chekechea kwa mchepuo wa Kingereza ya Betheli Mission na kuadhimisha miaka 25 ya Kanisa la Sabato katika kuendesha shule ya Msingi ya Betheli Mission.

Amesema kuwa Hakuna uwekezaji mkubwa na wa maana katika jamii kama uwekezaji katika elimu.

"Tunatambua mchango mkubwa ambao sekta binafsi inafanya katika kuendeshaa elimu ya nchi yetu." Amesema Prof. Mkumbo

Pia amewashukuru taasisi za dini hapa nchini wanaowekeza katika elimu kwa kazi kubwa wanayoifanya katika sekta ya elimu kwa sababu wanaisaidia serikali kuandaa taifa la kesho kupitia kwa vijana hao.

Amelishukuru kanisa la Sabato na shule hiyo kwa uwekezaji katika suala la maadili ambayo ni changamoto kubwa kwa sasa hasa kwa vijana. Amesema wao hawatoi elimu tuu bali wameweka msingi mkubwa katika suala la maadili.

Pia ametoa pongezi kwa kuunga mkono sera ya serikali ya kutokuwa na ubaguzi, kwa kuchukua watoto wa dini zote bila ubaguzi.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Shule ya Betheli, Emmanuel Mshana amesema kuwa shule ya Betheli Mission ni tofauti na shule nyingi kwa sababu wamejikita katika maadili na kuandaa watoto kwa maisha ya baadae.

"Mara nyingi watu wanaangalia maisha ya sasa tu, lakini sisi tunaamini kwamba kuna maisha baada ya kifo pia, huyu mtoto anaandaliwaje, kwamba baada ya hapa imani inatuambia kunapepo, kuna kwenda mbinguni, je huyu mtoto atafika?" Ameeleza naa Kuhoji Mshana.

Mshana ameeleza maana ya neno Betheli 'get to heven' yaani lango la mbinguni. 
Pia amemuomba Waziri Kibali ca kujenga Uzio wa Ukuta katika eneo la Makaburi lililopo karibu na eneo la shule ya Betheli Mission.

Amesema walishaomba kibali cha kujenga uzio katika eneo la maburi na Mhandisi alishafik eneo hilo lakini kibali kimekwama bila kuelezwa ni nini kimekwamisha. Amesema Uongozi wa shule upo teyari kujenga uzio katika eneo la Mbele ya makaburi na kuweka geti ili kuwe na muonekano mzuri eneo hilo.

Akizungumzia shule hiyo Mwenyekiti wa kanisa la Sabato Tanzania, Mchungaji Jurdon Mogela amesema kuwa wanakazi kubwa ya kuelimisha watoto kwenye maeneo matatu.

Ametaja maeneo hayo kuwa kuelimisha kiakili, ambapo watoto lazima wawe na akili kwani ni taifa la kesho, kimwili ambapo wanawapa lishe bora ili waweze kufanya vizuri madarani lakini pia wanawaelimisha kiroho kwamba lazima wawe na maadili mema.

Amesema taifa lisilo na maadili ni taifa mfu. "Tukiwa na vijana walioelimishwa vizuri watakuwa na hofu ya Mungu, lakini pia taifa litakuwa limejengaa msingi mzuri wa maadili popote wanawaweza kuwa watumishi waadilifu na popote."

Ikumbukwe kuwa Mahafali ya 19 ya wanafunzi wa Darasa la saba ilianzia 2017 pale walipoanza darasa la kwnza na leo Septemba tatu wanahitimu wakiwa32 Wasichana saba na wavulana 32.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...