Na Karama Kenyunko Michuzi TV

SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  (COSTECH) na kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hapa nchini,wametoa kiasi cha sh Bilioni 1.29 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi saba ya kitafiti kwa watafiti walioshinda maombi ya kufanya Utafiti kwenye nyanja ya Elimu, Kilimo,Afya na Uvuvi, kupitia Teknolojia ya kisasa.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya siku tatu ya watafiti wanufaika wa mradi huo, leo Septemba Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema fedha hizo zinatokana na tengeo katika bajeti kuu ya serikali pamoja na michango ya washirika wa maendeleo hususan Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Utafiti la Canada (IDRC) na Shirika la Maendeleo la Taifa la Norway (NORAD).

Amesema, matokeo ya utafiti utakaofanyika  kupitia ufadhili uliotolewa Utaimarisha ufaulu katika somo la hisabati kwa shule za msingi na sekondari huku  matumizi ya teknolojia zinazoibukia  yakitarajiwa kuongezeka hususan matumizi ya akili bandia katika kuchagiza maendeleo katika sekta za Kilimo, Uvuvi, Afya, Elimu, na Manunuzi serikalini.
 
"Nimefarijika kuona tafiti zimejikita katika maeneo muhimu ya jamii na yanashirikisha sekta husika, kipekee niwapongeze TAKUKURU ambao mmeshirikiana na vyuo kuingia katika ushindani na kushinda  kupata ufadhili Hivyo nasisitiza watafiti kuhusisha wadau wa sekta husika na tafiti mnazofanya na kuzingatia vipaumbele vya tafiti kitaifa( National Reserch Agenda)", Amesema Prof. Nombo

Amesema Serikali imeendelea kuongeza rasilimali fedha, kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili kuvutia wadau wengine wa Maendeleo ndani na nje ya nchi kuwekeza katika shughuli za utafiti na ubunifu nchini.
 
“Mazingira rafiki yameleta ambao umewezesha Serikali katika kipindi cha miaka mitano (2019-2022), kugharamia jumla ya miradi 49 ya utafiti, iliyojumuisha zaidi ya watafiti 235 kutoka Taasisi za Elimu ya Juu na zile za Utafiti na Maendeleo nchini,” amesema Prof Nombo

Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dkt. Amos Nungu amesema, kupitia mashirikiano hayo yaliyopo, COSTECH imefanikiwa kuleta fedha za utafiti hapa nchini zenye thamani ya takribani Sh. bilioni 9 kwa kipindi cha miaka minne. Fedha hizi zi
 
Akizungumia watafiti walioshinda katika mradi huo, Dkt. Nungu amesema, katika mchakato wa kupata washindi, watafiti 92 waliomba kufanya tafiti hizo,lakini baada ya mapitio ya awali, tafiti 57 zilikidhi vigezo vya kupelekwa kwa wataalam na baadae miradi saba ilichaguliwa kwa kuzingatia ufaulu wa juu zaidi.

"Ilikuwa kazi ngumu sana kuwapata watafiti hawa,na wanakwenda kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha wanafanikisha kufanya utafiti huo,"alisema Dk Nungu.

Dkt Nungu amesema kila taasisi na mshindi wake watakabidhiwa sh milioni 150, kwa ajili ya kukamilisha tafiti aliyoiomba,huku akisisitiza kila mtafiti na taasisi yake anapaswa kuzingatia vigezo na masharti katika fedha walizokabidhiwa.

Naye, Manyama Venance mmoja wa watafiti walioshinda, Afisa kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU),amesema wao kushirikiana na chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),wamekuja na utafiti wa kutumia akili bandia kuweza kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mifumo ya manunuzi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.

"Kumekuwa na tatizo kubwa la rushwa na ubadhilifu wa fedha za maendeleo na tafiti zimeonyesha fedha nyingi zinapotea katika mchakato wa manunuzi,"alisema Venance.

Kutokana na hilo utafiti huo wa kutumia akili bandia,utaiwezesha TAKUKURU kubaini viashiria vya rushwa katika maeneo mbalimbali wakati mchakato wa manunuzi unaendelea.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akikabidhi hundi ya zaidi ya Bilioni 1 ya ufadhili wa vikundi 9 vya utafiti

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akizungumza na wadau wa tafiti wakati wa hafla ya  kufunga mafunzo ya siku tatu ya watafiti wanufaika wa miradi saba ya kitafiti iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Septemba Mosi, 2023.
Mkurugenzi  Mkuu  wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dkt. Amos Nungu akizungumza na wadau wa tafiti wakati wa hafla ya  kufunga mafunzo ya siku tatu ya watafiti wanufaika wa miradi saba ya kitafiti iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Septemba Mosi, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...