Na Jane Edward, Arusha

Wataalamu wa fani ya misitu hapa nchini wanaotarajiwa kuingia Kwenye ajira wametakiwa kuwa na ubunifu wa teknolojia ya ufumbuzi wa kutafuta suluhisho la kudumu la kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia nchi katika maeneo yaliyo hifadhiwa yakiwemo wanyama pori na misitu.

Ambapo mimea vamizi inaendelea kuwa tishio hapa nchini na kwamba mimea hiyo inatajwa kuchangia wanyama pori kukosa malisho ya uhakika.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa idara ya misitu na nyuki Wizara ya maliasili na utalii Deusdedith Bwoyo katika chuo cha misitu Olmotonyi kilichopo Mkoani Arusha.

Amesema kuwa katika sekta ya misitu ni katika kusimamia kujenga uwezo kwa wataalamu wa misitu ambapo kwa Tanzania ni hekta takribani Milioni 48.

Amesema katika maeneo yanayotolewa elimu kuhusu misitu wanaendelea kuyaboresha ambapo mikakati mingine ni kuweka mabweni kwa wanafunzi na kuweka miundombinu rafiki.

Amesema mikakati ni kusimamia misitu ili iwe na faida kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae ambapo moja ya mikakati stahili ni kujenga uwezo wa kupata wataalamu wa kuhifadhi misitu na bila misitu uhifadhi utaenda vibaya.

"Wataalamu zaidi ya elfu kumi wanahitajika ili kuangalia misitu ili kuweza kuendelea kuwa na misitu yenye tija"Alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha misitu Olmotonyi Dokta Joseph Makero amesema  katika swala la Mabadiliko ya tabia nchi tayari vijana wanaozalishwa na Chuo hicho wamejengewa uwezo wa kukabiliana na Mabadiliko hayo kwa manufaa ya Nchi.

Amebainisha kuwa kwa mwaka huu wamejipanga kutumia utalii ikolojia ambao unahusisha fani ya misitu bila kukata wala kufyeka na wamejipanga ndani ya miaka miwili kuanzisha kozi maalumu ya kuwatoa wahitimu katika fani hiyo ya mambo ya ikolojia.

Amesema kuwa wahitimu wengi wa Chuo hicho ni kutoka ndani ya nchi ambapo walikuwa ni mia nane lakini mipango ni kupata wahitimu kutoka nje kama ilivyokuwa hapo Awali.

Mkurugenzi wa idara ya misitu na nyuki Wizara ya maliasili na utalii Deusdedith Bwoyo akifafanua jambo.
Mkuu wa Chuo cha misitu Olmotonyi Dokta Joseph Makero akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...