Na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA wa jijini Tanga, Sultan Salim amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati mchakato wa upatikanaji wa mshindi wa zabuni wa eneo la Jamhuri Pack 'Forodhani' jijini humo.

Kauli hiyo imekuja baada ya mfanyabiashara huyo kudai amedhulumiwa haki yake kutokana na mchakato ulivyofanywa hadi kupatikana mshindi kuna taratibu na kanuni zimekiukwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Salim alidai kuwa kinachoonekana wanataka kumnyima haki yake kwa makusudi kwani alistahili kushinda zabuni hiyo kutokana na dau kubwa alilotoa.

"Agosti Mosi, mwaka huu niliomba zabuni hiyo ya Jamhuri Pack na nashukuru nilishinda kwakuwa dau langu la Sh. milioni 2.2 hakuna ambaye alilifikia siku hiyo ya ufunguzi wa zabuni hiyo," alisema na kuongeza;

"Lakini chakushangaza Halmashauri ya Jiji la Tanga ilivyofika Agosti 8, mwaka huu wakatoa makusudio ya upangaji na kumtangaza Ali Salim Mohamed kuwa mshindi kwa dau la sh. mil. 2.3 wakati siku ya ufunguzi tenda hiyo alitoa dau la Sh.milioni 1.3 ".

Alidai anashangaa kuona mpinzani wake kutangazwa ameshinda tenda hiyo wakati siku ya ufunguzi alitoa dau dogo na yeye alitoa kubwa kitu ambacho kinampa maswali mengi bila majibu.

Akifafanua zaidi alisema baada ya sintofahamu hiyo aliandika barua kwenda halmashauri kupinga matokeo hayo pamoja na kuweka zuio lakini majibu yakabaki vile vile.

"Halmashauri ilijibu kwa kutilia mkazo matokeo yao ya awali waliyoyatoa na hata nilipoandika barua ya pili kwao na kuambatanisha na nyaraka zote za mchakato mzima ulivyoanza hadi kunionesha mimi ndiye nilipaswa kuwa mshindi, haikusaidia kitu kwani halmashauri ilikataa kupitia nyaraka zangu," alidai Salim.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...