Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

Serikali imeanza Uchunguzi Maalumu wa kubaini mapungufu mbalimbali katika Viwanja vyote vya Ndege nchini ili kubaini changamoto hizo na kuweza kuzifanyia kazi ikiwemo Mapungufu ya Kimfumo,Utendaji na Upungufu wa Miundombinu ili kuweza kuboresha sehemu husika lengo ikiwa kurahisisha uingiaji na utokaji wa wageni ikiwemo watalii wanoukuja nchini kwa shughuli za utalii ambao uiingizia nchi kiasi kikubwa cha fedha sambamba na kudhibiti uhalifu unaotokea katika Viwanja vya Ndege ikiwemo utoroshaji wa vito vya thamani,mnyororo wa upitishaji na uingiaji wa dawa za kulevya na uingiaji nchini kwa wageni bila kufuata sheria na taratibu za kiuhamiaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama ambapo kamati hiyo ilitembelea na Kukagua Mifumo ya Uhamiaji Mtandao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Ujenzi wa Chuo cha Uhamiaji Kitogani na Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Mjini Magharibi Mazizini.

‘Mbali ya kazi nzuri ambazo zinafanywa na Uhamiaji lakini kuna maeneo tunataka kupeleka nguvu zaidi hasa maeneo ambayo kwanza ni sura ya nchi,malango makuu ya kuingilia kama hapa tulipo katika maeneo ya Viwanja vya Ndege,mtu akija Tanzania sura ya nchi inamuonyesha anapopokelewa katika viwanja vya ndege,haipendezi mgeni akija hapa nchini apange mstari mrefu,mara viyoyozi havifanyi kazi ndio maana serikali kuna uchunguzi maalumu tunafanya ili kuweza kubaini mapungufu hayo na kuyafanyia kazi katika Viwanja vyote vya ndege nchini.’ Alisema Waziri Masauni

Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama,Vicent Mbogo amesema ni muhimu mapungufu hayo katika viwanja vya ndege yakafanyiwa kazi huku akisifu juhudi za serikali zote mbili katika kuiletea Zanzibar maendeleo ambapo alisema Zanzibar ni nchi ya utalii ni vyema huduma malango yan chi zikaboreshwa.

‘Zanzibar imeendelea kwa kasi kubwa pamoja na maendeleo haya ya miundombinu katika uwanja wa ndege ambapo sasa yanasomana na kule Tanzania Bara tumeona maendeleo yanafanyika katika viwanja vyetu ambavyo ndio maingilio ya watalii ambao wanatuletea fedha nyingi hapa nchini,napenda kwapongeza Marais wetu,Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt.Hussein Ali Mwinyi wanafanya kazi kubwa sana kuiletea nchi yetu maendeleo’alisema Mbogo

Nae Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan alitaja jinsi miradi ya maendeleo ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 ilivyokamilika ikiwemo Ujenzi wa Ofisi ya Uhmiaji mkoa wa Mjini Magharibi,Mkoa wa Kusini Pemba,Ukarabati wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar,Ukarabati wa Nyumba ya Makazi ya Askari Ndugu Kitu Chake Chake Pemba na Ukarabati wa Nyumba Mbili za Makaazi ya Askari Mtemani Wete na Pemba ambapo imekamilika kwa asilimia mia moja huku gharama yake ikiwa ni kiasi cha Shilingi Bilioni1.9 .

Afisa Mfawidhi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji,Abdul Rahman Khamis Juma akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama jinsi shughuli za uhamiaji ikiwepo uingiaji na utokaji wa raia na wageni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.Wakwanza kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni na wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati,Vicent Mbogo.Picha na Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Mkuu wa Kitengo cha Majengo Uhamiaji Zanzibar, Mrakibu Msaidizi, Mvita Yussuf akitoa maelezo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ,Ulinzi na Usalama,Vicent Mbogo(kushoto) jinsi Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi unavyoendelea.Katikati ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan.Picha na Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...