Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa, tarehe 17 Machi 2025, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Bi. Kwakwa alifika Ikulu kuaga rasmi baada ya kustaafu kufanya kazi Benki ya Dunia kwa muda wa miaka 35. Kwa upande wake Rais Dkt. Samia amemshukuru kwa ushirikiano aliouonyesha kwa Tanzania kwa muda wote wa uongozi wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...