Muandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeanza rasmi utambulisho wa jezi maalum na vifaa vitakazotumiwa na washiriki wa mbio hizo kwa kuzikabidhi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wadhamini wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma.
Zoezi hilo liloanza leo jijini Dar es Salaam liliongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Rayson Foya, likianzia kwa mmoja wa wadhamini muhimu mbio hizo Kampuni ya Bima ya Sanlam huku likitarajiwa kuendelea kwa wadau wengine wengi wakiwemo wadhamini, taasisi wanufaika wa mbio hizo, wadau wa mchezo huo pamoja na viongozi waandamizi wa serikali.
Hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo imefanyika leo makao makuu ya Kampuni ya Bima ya Sanlam jijini Dar es Salaam ambapo ilishuhudiwa Bw Foya alieambatana na baadhi ya maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki hiyo Bw Godwin Semunyu wakipokelewa na mwenyeji wao Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bima ya Sanlam, Bw Julius Magabe sambamba na maofisa wengine waandamizi wa kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Bw Foya pamoja na kuishukuru kampuni ya Bima ya Sanlam kwa kuwa wadhamini muhimu wa mbio hizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020, alisisitiza kuhusu umuhimu na nafasi wa wadau hao katika kufanikisha kusudi la mbio hizo la kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kupanua ufadhili wa wakunga hadi kufikia wakunga 200 pamoja na kuanzisha mpango mpya wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 kwa ajili ya watoto wenye changamoto za usonji (autism) nchini.
“NBC Dodoma Marathon sio tu tukio la kimichezo bali pia ni jukwaa la matumaini ya maisha kwa watanzania. Ushiriki wa Sanlam kwenye mbio hizi kupitia udhamini wao umekuwa ni chachu muhimu katika kufanikisha kusudi leo hilo mihumu. Leo hii tunawakabidhi jezi hizi zenye mvuto na ubora wa hali ya juu wadau wetu wa Sanlam ikiwa namna ya kuheshimu mchango wao huo kipekee kabisa na tutaendelea na zoezi hili kwa wadau wetu wengine wengi ikiwa ni ishara ya sisi kutambua mchango wao kwetu kwa faida ya taifa letu,’’ alisema
Kwa upande wake Bw Magabe pamoja na kupongeza ubora na ubunifu wa jezi hizo, aliishukuru benki hiyo kwa namna inavyoandaa tukio hilo kwa weledi wa hali ya juu hatua ambayo imeongeza mvuto wake kiasi cha kuwavutia maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.
“Zaidi tunawapongeza NBC kwa namna ambavyo wamekuwa wakilitumia tukio hilo kukusanya fedha kwa ajili ya kufanikisha makusudi muhimu ya mbio hizi. Ni kupitia kuridhishwa kwetu na nia pamoja na uratibu wa mbio hizo ndio imekuwa sababu ya Sanlam Insurance kuendelea kuziunga mkono kama wadau muhimu tangu kuanzishwa kwake huu ukiwa ni msimu wake wa sita na tunaahidi kuendelea kuziunga mkono zaidi katika misimu mingine ijayo,’’ alisema.
Akizungumzia maandalizi ya mbio hizo, Bw Semunyu alisema mwitikio wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi ni mkubwa huku usajili wa mbio hizi ukiendelea kupitia tovuti ya www.events.nbc.co.tz ambapo washiriki wanatakiwa kuchangia kiasi cha TZS 45,000 kwa usajili wa mtu mmoja mmoja au 42,000 kwa usajili wa kikundi chenye idadi ya watu 30 au zaidi.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Rayson Foya (wa tatu kushoto) akikabidhi moja ya jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bima ya Sanlam, Bw Julius Magabe (wa tatu kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kama mdhamini muhimu wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni maofisa waandamizi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Rayson Foya (kushoto) akikabidhi moja ya jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bima ya Sanlam, Bw Julius Magabe (kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kama mdhamini muhimu wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Rayson Foya (kushoto) akikabidhi moja ya jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bima ya Sanlam, Bw Julius Magabe (kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo kama mdhamini muhimu wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bima ya Sanlam, Bw Julius Magabe (katikati) akizungumza na wageni wake kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambao ni waandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Bw Rayson Foya ( wa tatu kulia) wakati maofisa hao walipotembelea makao makuu ya kampuni ya Bima ya Sanlam kwa ajili ya kumkabidhi jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...