Na Mwandishi Wetu
Tume ya Ushindani (FCC) imekutana na wadau wa uzalishaji wa ndani wa Saruji kwa kwa ajili ya kujadiliana kuhusiana hali uzalishaji Saruji pamoja na kulinda soko.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Khadija Ngasongwa amesema FCC kuwa kutukatana na wadau hao na kufanya mahojiano ya kutaka kujenga soko hilo katika ushindani sambamba na kumlinda mlaji.
Khadija amesema kuwa baada ya kufanya majadiliano hayo ndipo watapata mwanga kutoa suluhisho katika ushindani wa saruji katika soko na kwa mlaji.
Amesema wazalishaji wa Saruji waliweka taarifa (Notice) ya kupanda kwa Bei ya Saruji hivyo lazima kuangalia kwa mizani ya hali hiyo pamoja kuangalia gharama za uendeshaji pamoja gharama za malighafi.
"Katika majadiliano haya matokeo yake yatakuwa ya kujenga afya katika soko la bidhaa ya saruji pamoja mlaji kulindwa kwenye upatikanaji bidhaa hiyo"amesema
Ngasongwa
Sekta ya uzalishaji wa Saruji ni muhimu katika Tanzania nchi zinazoendelea ikizingatiwa miongozo na dira yetu 2050 katika sekta ya ujenzi katika sehemu nyingi za viwanda vitategemea wazalishaji wa Seruji.
Amesema jukumu la FCC ni muhimu kukaa na kujadili na sera na miongozo na kufanya mahojiano hayo kuchukuliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara atatoa miongozo kwa wadau hao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC,Khadija Ngasongwa akizungumza na wadau wa Wazalishaji wa Ndani wa Saruji wakati walipokutana kujadiliana kuhusiana hali ya Soko ya bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC,Khadija Ngasongwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na ofisi hiyo kufanya majadiliano na Wazalishaji wa Ndani wa Saruji jijini Dar es Salaam.
FCC katika kikao cha Wazalishaji wa Ndani wa Saruji jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya matukio katika picha ya katika kikao cha majadiliano.





.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...