Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara ya Nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kasi ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 15 kwa kila jimbo nchini ili kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Subira Mgalu ametoa kauli hiyo katika ziara ya Kamati hiyo walioambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika vitongoji vya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Mgalu amesema kuwa Bunge liliidhinisha bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya kupeleka umeme katika vitongoji 15 kwa kila jimbo Tanzania Bara kupitia REA, mpango ambao umeanza kuonyesha matokeo chanya katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Amesema katika Mkoa wa Shinyanga pekee, umeme tayari umefika katika vitongoji 90, jambo linaloonyesha juhudi kubwa za Serikali katika kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata huduma muhimu ya nishati.
“Tunaipongeza Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huu kupitia REA. Kasi ya usambazaji wa umeme vitongojini inaendelea kuleta matumaini makubwa kwa wananchi na kuboresha maisha yao,” amesema Mhe. Mgalu.
Aidha, ameihimiza REA kuendelea kuongeza juhudi katika kupeleka umeme kwenye taasisi muhimu za umma kama zahanati, vituo vya afya, shule za msingi na sekondari, miradi ya maji pamoja na taasisi za dini ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na huduma hiyo.
Amesisitiza Wizara hiyo kusimamia wananchi kuunganishiwa huduma ya umeme katika vitongoji kwa gharama ya Sh.27,000 ili kutimiza maono ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha umeme unafika katika vitongoji vyote nchini ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome amesema utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme katika vitongoji mkoani Shinyanga unaendelea vizuri na tayari umeanza kuleta manufaa kwa wananchi, hususan katika shughuli za uzalishaji na huduma za kijamii, hali inayoleta tabasamu kwa wananchi.
Amesema ataendelea kushirikiana na Waziri wa Nishati, Mhe.Deogratius Ndejembi, kusimamia maelekezo ya Rais kuhakikisha umeme unawashwa katika vitongoji vyote, sambamba na kauli mbiu ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ya 'Salome Makamba, Washa umeme'.
Katika ziara hiyo, Kamati ya Bunge pia ilikagua na kuwasha umeme katika Zahanati ya Mine iliyopo Jimbo la Msalala, pamoja na kuwasha huduma ya umeme katika mashine ya kusaga na kukoboa katika Jimbo la Kahama Mjini, huduma zilizopatikana kupitia mradi wa kusambaza umeme vitongoji 15 kwa kila jimbo (HEP IIA)..jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...